Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Yos 16

16
Nchi ya Efraimu
1 # Hes 33:45 Kura ya wana wa Yusufu ilianza kutoka mto wa Yordani hapo Yeriko, hapo penye maji ya Yeriko upande wa mashariki, maana, ni hiyo nyika, kukwea kutoka Yeriko kati ya hiyo nchi ya vilima mpaka Betheli; 2#Mwa 28:19; Yos 18:13; Amu 1:26kisha ikatoka huko Betheli kwendelea Luzu, kisha ikaendelea hata kuufikilia mpaka wa Waarki mpaka Atarothi; 3#Yos 18:13; 21:22; 2 Nya 8:5; 1 Nya 7:28; 1 Fal 9:15kisha ikatelemkia upande wa magharibi hata kuufikilia mpaka wa Wayafleti, hata mpaka wa Beth-horoni ya chini, hata kufikilia Gezeri; na matokeo yake yalikuwa hapo baharini. 4#Yos 17:14Na wana wa Yusufu, Manase na Efraimu, walitwaa urithi wao. 5#Yos 18:13; 2 Nya 8:5Na mpaka wa wana wa Efraimu kwa kuandama jamaa zao ulikuwa hivi; mpaka na urithi wao upande wa mashariki ulikuwa ni Ataroth-adari, hata Beth-horoni wa juu; 6#Yos 17:7kisha mpaka ukatokea kwendelea upande wa magharibi huko Mikmeta upande wa kaskazini; kisha mpaka ukazunguka kwendea upande wa mashariki hata Taanath-shilo, kisha ukaendelea upande wa mashariki wa Yanoa; 7#1 Nya 7:28kisha ulitelemka kutoka Yanoa hata Atarothi, na Naara, kisha ukafikilia Yeriko, na kutokea hapo penye mto wa Yordani. 8#Yos 17:9; 19:28Kutoka hapo Tapua mpaka ukaendelea upande wa magharibi hata kijito cha Kana; na matokeo yake yalikuwa baharini. Huo ndio urithi wa hao wana wa Efraimu kwa kuandama jamaa zao; 9pamoja na ile miji iliyotengwa kwa ajili ya wana wa Efraimu katikati ya urithi wa hao wana wa Manase, miji yote pamoja na vijiji vyake. 10#Amu 1:29; Yos 15:63; 1 Fal 9:16,20,21; Mwa 9:25; Yos 17:12,13Nao hawakuwatoa Wakanaani waliokuwa Wakikaa Gezeri; lakini hao Wakanaani waliketi kati ya Efraimu, hata hivi leo, wakawa watumishi wa kufanya kazi za shokoa.

Iliyochaguliwa sasa

Yos 16: SUV

Kuonyesha

Shirikisha

Nakili

None

Je, ungependa vivutio vyako vihifadhiwe kwenye vifaa vyako vyote? Jisajili au ingia