Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Yos 15

15
Nchi ya Yuda
1 # Hes 34:3; 33:36 Kura ya kabila ya wana wa Yuda kwa kuandama jamaa zao ilikuwa kufikilia hata mpaka wa Edomu, hata bara ya Sini upande wa kusini, huko mwisho upande wa kusini. 2Mpaka wao wa kusini ulikuwa kutoka mwisho wa Bahari ya Chumvi, kutoka ile hori ielekeayo kusini; 3nao ukaendelea upande wa kusini wa kukwea kwenda Akrabimu, kisha ukaendelea hata Sini, kisha ukaenda upande wa kusini wa Kadesh-barnea, kisha ukaendelea karibu na Hesroni, kisha ukafikilia Adari, na kuzunguka kwendea Karka; 4#Hes 34:5; Mwa 15:18; 1 Fal 8:65kisha ukaendelea hata Azmoni, na kutokea hapo penye kijito cha Misri; na matokeo ya huo mpaka yalikuwa baharini; huu ndio mpaka wenu wa upande wa kusini. 5Na mpaka wa upande wa mashariki ulikuwa Bahari ya Chumvi, hata mwisho wa mto wa Yordani. Na mpaka wa upande wa kaskazini ulikuwa kutoka pale penye hori ya baharini mwisho wa mto wa Yordani; 6#Yos 18:17na huo mpaka ukaendelea hata Beth-hogla, kisha ukaendelea upande wa kaskazini wa Beth-araba; kisha mpaka ukaendelea hata jiwe la Bohani mwana wa Reubeni; 7#Yos 7:26; Isa 65:10; Hos 2:15; 2 Sam 17:17kisha mpaka ukaendelea hata Debiri kutoka bonde la Akori, vivyo ukaendelea upande wa kaskazini, kwa kuelekea Gilgali, iliyo mkabala wa kukwelea kwenda Adumimu, ulio upande wa kusini wa mto; kisha huo mpaka ukaendelea hata ukafikilia maji ya Enshemeshi, na matokeo yake yalikuwa hapo Enrogeli; 8#Yos 18:16,28; 2 Fal 23:10; Yer 19:2,6; Amu 1:21; 19:10; 2 Sam 5:18kisha mpaka ukaendelea karibu na bonde la mwana wa Hinomu, na kufikilia ubavuni mwa huyu Myebusi upande wa kusini (ndio Yerusalemu); kisha mpaka ukaendelea hata kilele cha mlima ulio pale mkabala wa bonde la Hinomu upande wa magharibi, lililo pale mwisho wa bonde la Warefai upande wa kaskazini; 9#1 Nya 13:6; Amu 18:12kisha mpaka ulipigwa kutoka juu ya mlima huo hata kufikilia chemchemi ya maji ya Neftoa kisha ukatokea hata miji ya kilima cha Efroni; kisha mpaka ulipigwa hata kufikilia Baala (ndio Kiriath-yearimu); 10#Mwa 38:13; Amu 14:1kisha mpaka ukazunguka kutoka Baala kwendelea upande wa magharibi hata kilima Seiri, kisha ukaendelea hata upande wa mlima wa Yearimu upande wa kaskazini (huo ndio Kesaloni), kisha ukatelemkia Beth-shemeshi, na kwendelea karibu na Timna; 11#Yos 19:43; 1 Sam 5:10kisha mpaka ukatokea hata kufikilia upande wa Ekroni upande wa kaskazini; tena mpaka ulipigwa hata Shikroni, na kwendelea hata kilima cha Baala, kisha ukatokea hapo Yabneeli; na matokeo ya mpaka yalikuwa baharini. 12#Hes 34:6; Kum 11:24; Eze 47:20Na mpaka wa upande wa magharibi ulifikilia hata bahari kubwa, na mpaka wake. Huo ndio mpaka wa wana wa Yuda kwa kuzunguka kote kote sawasawa na jamaa zao.
Kalebu Aichukua Milki yake
13 # Yos 14:13; Mwa 23:2 Kisha alimpa huyo Kalebu mwana wa Yefune sehemu kati ya wana wa Yuda, kama BWANA alivyomwamuru Yoshua, maana ni Kiriath-arba, ni huyo Arba aliyekuwa babaye Anaki (huo ndio Hebroni). 14#Amu 1:10; Hes 13:22Huyo Kalebu aliwafukuza watoke hapo hao wana watatu wa Anaki, nao ni Sheshai, na Ahimani, na Talmai, wana wa Anaki. 15#Yos 10:38Kisha akakwea kutoka huko ili kuwaendea wenyeji wa Debiri; jina la Debiri hapo kwanza lilikuwa Kiriath-seferi. 16Kalebu akasema, Yeye atakayeupiga Kiriath-seferi na kuutwaa, mimi nitampa Aksa binti yangu awe mkewe. 17#Amu 3:9; Hes 32:12; Yos 14:6Naye Othnieli mwana wa Kenazi, nduguye Kalebu, aliutwaa; basi akampa Aksa binti yake awe mkewe. 18#Amu 1:14; Mwa 24:64; 1 Sam 25:23Kisha ikawa, hapo huyo mwanamke alipokwenda kwa mumewe, akamtaka aombe shamba kwa baba yake; akashuka katika punda wake; Kalebu akamwuliza, Wataka nini? 19#Mwa 33:11Huyo mwanamke akasema, Nipe baraka; kwa kuwa umeniweka katika nchi ya kusini, unipe na chemchemi za maji pia. Ndipo akampa chemchemi za maji ya juu, na chemchemi za maji ya chini.
Miji ya Yuda
20 # Mwa 49:8-12; Kum 33:7 Huu ndio urithi wa kabila ya wana wa Yuda sawasawa na jamaa zao.
21 # Mwa 35:21 Miji ya mwisho ya kabila ya wana wa Yuda upande wa kuelekea mpaka wa Edomu katika nchi ya Negebu ilikuwa ni Kabseeli, na Ederi, na Yaguri; 22na Kina, na Dimona, na Adada; 23na Kedeshi, na Hazori, na Ithnani; 24#1 Sam 15:4na Zifu, na Telemu, na Bealothi; 25na Hazor-hadata, na Kerioth-hezroni (ndio Hazori); 26na Amamu, na Shema, na Molada; 27na Hasar-gada, na Heshmoni, na Bethpeleti; 28na Hasarshuali, na Beer-sheba, na Biziothia; 29na Baala, na Iyimu, na Esemu; 30na Eltoladi, na Kesili, na Horma; 31#Yos 19:5; 1 Sam 27:6; 30:1; 1 Nya 12:1na Siklagi, na Madmana, na Sansana; 32#Neh 11:29na Lebaothi, na Shilhimu, na Aini, na Rimoni; miji hiyo yote ni miji ishirini na kenda, pamoja na vijiji vyake.
33 # Yos 19:41; Hes 13:23 Katika nchi ya Shefela, Eshtaoli, na Sora, na Ashna, 34na Zanoa, na Enganimu, na Tapua, na Enamu; 35#Yos 10:3,5; 12:15; 1 Sam 17:1; Yos 10:10na Yarmuthi, na Adulamu, na Soko, na Azeka; 36#1 Sam 17:52na Shaarimu, na Adithaimu, na Gedera, na Gederothaimu miji kumi na minne, pamoja na vijiji vyake.
37Senani, na Hadasha, na Migdal-gadi; 38#2 Fal 14:7na Dilani, na Mispe, na Yoktheeli; 39#Yos 10:3; 2 Fal 18:14; 19:8; 2 Nya 11:9; 2 Fal 22:1; Yos 12:12na Lakishi, na Boskathi, na Egloni; 40na Kaboni, na Lamasi, na Kithilishi; 41na Gederothi, na Beth-dagoni, na Naama, na Makeda; miji kumi na sita, pamoja na vijiji vyake.
42Libna, na Etheri, na Ashani; 43na Yifta, na Ashna, na Nesibu; 44na Keila, na Akizibu, na Maresha; miji kenda, pamoja na vijiji vyake.
45Ekroni, pamoja na miji yake na vijiji vyake; 46#Yos 13:3; 1 Sam 5:1,6kutoka huko Ekroni mpaka baharini, yote iliyokuwa upande wa Ashdodi, pamoja na vijiji vyake.
47 # Mwa 15:18; Hes 34:6 Ashdodi, na miji yake na vijiji vyake; na Gaza, na miji yake na vijiji vyake; mpaka kijito cha Misri, na bahari kubwa, na mpaka wake.
48Na katika nchi ya vilima, Shamiri, na Yatiri, na Soko; 49na Dana, na Kiriath-sana (ambao ni Debiri); 50na Anabu, na Eshtemoa, na Animu; 51#Yos 10:41; 11:16na Gosheni, na Holoni, na Gilo; miji kumi na mmoja, pamoja na vijiji vyake.
52Arabu, na Duma, na Eshani; 53na Yanumu, na Beth-tapua, na Afeka; 54#Mwa 23:2; Yos 14:15; Amu 1:10na Humta, na Kiriath-arba (ndio Hebroni), na Siori; miji kenda, pamoja na vijiji vyake.
55Maoni, na Karmeli, na Zifu, na Yuta; 56na Yezreeli, na Yokdeamu, na Zanoa; 57na Kaini, na Gibea, na Timna; miji kumi, pamoja na vijiji vyake.
58Halhuli, na Bethsuri, na Gedori; 59na Maarathi, na Bethanothi, Eltekoni; miji sita, pamoja na vijiji vyake.
60 # Yos 18:14; 1 Sam 7:1,2; 1 Nya 13:6 Kiriath-baali (ndio Kiriath-yearimu), na Raba; miji miwili, pamoja vijiji vyake.
61Huko nyikani, Betharaba, na Midini, na Sekaka; 62#1 Sam 23:29na Nibshani, na huo Mji wa Chumvi, na Engedi; miji sita, pamoja na vijiji vyake.
63 # Amu 1:8,21; 19:10-12; Hes 13:29; 2 Sam 5:6; 24:16,18; 1 Nya 11:4; 2 Nya 3:1; Zek 9:7 Tena katika habari ya Wayebusi, hao wenye kukaa Yerusalemu, wana wa Yuda hawakuweza kuwatoa; lakini hao Wayebusi walikaa pamoja na wana wa Yuda huko Yerusalemu hata hivi leo.

Iliyochaguliwa sasa

Yos 15: SUV

Kuonyesha

Shirikisha

Nakili

None

Je, ungependa vivutio vyako vihifadhiwe kwenye vifaa vyako vyote? Jisajili au ingia