Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Ayu 8

8
Bildadi Anena: Ayubu Astahili Kutubu
1Ndipo Bildadi huyo Mshuhi akajibu, na kusema,
2Wewe utanena maneno haya hata lini?
Maneno ya kinywa chako yatakuwa kama upepo mkuu hata lini?
3 # Mwa 18:25; Kum 32:4; Ayu 34:12; Dan 9:14 Je! Mungu hupotosha hukumu?
Au, huyo Mwenyezi hupotosha yaliyo ya haki?
4Kwamba watoto wako wamemfanyia dhambi,
Naye amewatia mkononi mwa kosa lao;
5Wewe ukimtafuta Mungu kwa bidii,
Na kumsihi huyo Mwenyezi;
6Ukiwa wewe u safi na mwelekevu;
Hakika yeye sasa angeamka kwa ajili yako,
Na kuyafanya makazi ya haki yako kufanikiwa.
7Tena ujapokuwa huo mwanzo wako ulikuwa ni mdogo,
Lakini mwisho wako ungeongezeka sana.
8 # Kum 4:32 Basi, uwaulize, tafadhali, vizazi vya zamani,
Ujitie kuyaangalia yale baba zao waliyoyatafuta;
9 # Mwa 47:9; Zab 39:5 (Kwani sisi tu wa jana tu, wala hatujui neno,
Kwa kuwa siku zetu duniani ni kivuli tu;)
10Je! Hawatakufunza wao, na kukueleza,
Na kutamka maneno yatokayo mioyoni mwao?
11Je! Hayo mafunjo yamea pasipo matope
Na makangaga kumea pasipo maji?
12 # Zab 129:6; Yer 17:6; Yak 1:10,11; 1 Pet 1:24 Yakiwa yakali mabichi bado, wala hayakukatwa,
Hunyauka mbele ya majani mengine.
13 # Ayu 11:20; 18:14; Zab 112:10; Mit 10:28; Isa 33:14; Mt 24:51; Lk 12:1,2 Ndivyo ulivyo mwisho wa hao wamsahauo Mungu;
Na matumaini yake huyo mbaya huangamia;
14Uthabiti wake utavunjika,
Na matumaini yake huwa ni nyuzi za buibui.
15 # Ayu 27:18 Ataitegemea nyumba yake, isisimame;
Atashikamana nayo, isidumu.
16Yeye huwa mti mbichi mbele ya jua,
Nayo machipukizi yake huenea katika bustani yake.
17Mizizi yake huzonga-zonga chuguu,
Huangalia mahali penye mawe.
18 # Ayu 7:10; Zab 37:36 Lakini, aking’olewa mahali pake,
Ndipo patamkana, na kusema, Mimi sikukuona.
19 # Zab 113:7 Tazama, furaha ya njia yake ni hii,
Na wengine watachipuka kutoka katika nchi.
20 # Zab 37:24; 1 The 5:23,24 Tazama, Mungu hatamtupa mtu mkamilifu,
Wala hatawathibitisha watendao uovu.
21Bado atakijaza kinywa chako kicheko,
Na midomo yako ataijaza shangwe.
22Hao wakuchukiao watavikwa aibu;
Nayo hema yake mwovu haitakuwako tena.

Iliyochaguliwa sasa

Ayu 8: SUV

Kuonyesha

Shirikisha

Nakili

None

Je, ungependa vivutio vyako vihifadhiwe kwenye vifaa vyako vyote? Jisajili au ingia