Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Ayu 6

6
Ayubu Ajibu: Lalamiko langu ni la Haki
1Ndipo Ayubu akajibu na kusema,
2Laiti uchungu wangu ungepimwa,
Na msiba wangu kutiwa katika mizani pamoja!
3Kwa kuwa sasa ungekuwa mzito kuliko mchanga wa bahari;
Kwa hiyo maneno yangu yamekuwa ya haraka.
4 # Kum 32:23,42; Ayu 16:12-14; Zab 7:13; 18:14; 21:12 Kwa kuwa mishale ya huyo Mwenyezi i ndani yangu,
Na roho yangu inainywa sumu yake;
Vitisho vya Mungu vimejipanga juu yangu.
5Je! Huyo punda-mwitu hulia akiwa na majani?
Au, ng’ombe hulia malishoni?
6Je! Kitu kisicho na ladha yumkini kulika pasipo chumvi?
Au je, uto wa yai una tamu iwayo yote?
7Roho yangu inakataa hata kuvigusa;
Kwangu mimi ni kama chakula kichukizacho.
8Laiti ningepewa haja yangu,
Naye Mungu angenipa neno hilo ninalolitamani sana!
9Kwamba Mungu angekuwa radhi kuniseta;
Kwamba angeulegeza mkono wake na kunikatilia mbali!
10Hapo ndipo ningefarijika hata sasa;
Naam, ningejikuza katika maumivu yasiyoniacha;
Kwa kuwa sikuyakana maneno yake Mtakatifu.
11Nguvu zangu ni zipi, hata ningoje?
Na mwisho wangu ni nini, hata nisubiri?
12Je! Nguvu zangu ni nguvu za mawe?
Au mwili wangu, je! Ni shaba?
13Je! Si kwamba sina msaada ndani yangu.
Tena kwamba kufanikiwa kumeondolewa mbali nami?
14Kwake huyo atakaye kuzima roho inapasa atendewe mema na rafiki;
Hata kwake huyo aachaye kumcha Mwenyezi.
15Ndugu zangu wametenda udanganyifu kama kijito cha maji.
Mfano wa fumbi la vijito vipitavyo.
16Vilivyokuwa vyeusi kwa sababu ya barafu,
Ambamo theluji hujificha.
17Wakati vipatapo moto hutoweka;
Kukiwako hari, hukoma mahali pao.
18Misafara isafiriyo kwa njia yao hugeuka;
Hukwea kwenda barani, na kupotea.
19Misafara ya Tema huvitazama,
Majeshi ya Sheba huvingojea.
20Wametahayari kwa sababu walitumaini;
Wakaja huku, nao walifadhaika.
21 # Zab 38:11 Kwani sasa ninyi mmekuwa vivyo;
Mwaona jambo la kutisha, mkaogopa.
22 # Mdo 20:33 Je! Nilisema, Nipeni?
Au, Nitoleeni toleo katika mali yenu?
23Au, Niokoeni na mkono wa adui?
Au, Nikomboeni na mikono ya hao waoneao?
24 # Zab 39:1 Nifunzeni, nami nitanyamaa kimya;
Mkanijulishe ni jambo gani nililokosa.
25Jinsi yafaavyo maneno ya uelekevu!
Lakini kuhoji kwenu, je! Kumeonya nini?
26Je! Mwafikiri kuyakemea maneno?
Maana maneno ya huyo aliyekata tamaa ni kama upepo.
27Naam, mwapenda kuwapigia kura hao mayatima,
Na kufanya biashara ya rafiki yenu.
28Sasa basi iweni radhi kuniangalia;
Kwani hakika sitanena uongo usoni penu.
29Rudini, nawasihi, lisiwe neno la udhalimu;
Naam, rudini tena, neno langu ni la haki.
30 # Ayu 33:8-12; Yak 3:13 Je! Mna udhalimu ulimini mwangu?
Je! Makaakaa yangu hayatambui mambo ya madhara?

Iliyochaguliwa sasa

Ayu 6: SUV

Kuonyesha

Shirikisha

Nakili

None

Je, ungependa vivutio vyako vihifadhiwe kwenye vifaa vyako vyote? Jisajili au ingia