Ayu 36:26-33
Ayu 36:26-33 SUV
Tazama, Mungu ni mkuu, nasi hatumjui; Hesabu ya miaka yake haitafutiki. Kwani yeye huvuta juu matone ya maji, Yamwagikayo katika mvua kutoka kungeni mwake; Ambayo mawingu yainyesha Na kudondoza juu ya wanadamu kwa wingi. Naam, mtu aweza kuelewa na matandazo ya mawingu, Ngurumo za makao yake? Tazama, yeye huutandaza mwanga wake, umzunguke; Naye hufunika vilindi vya bahari. Kwani huwahukumu kabila za watu kwa njia hizi; Hutoa chakula kwa ukarimu. Yeye huifunika mikono yake kwa umeme; Na kuuagiza shabaha utakayopiga. Mshindo wake hutoa habari zake, Anayewaka hasira juu ya uovu.