Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Ayu 30

30
1Lakini sasa hao walio wadogo wangu hunifanyia mzaha,
Ambao baba zao niliwadharau hata kuwaweka na mbwa wa kundi langu.
2Naam, uwezo wa mikono yao utanifaa nini?
Watu ambao nguvu zao zimekoma.
3Wamekonda kwa uhitaji na njaa;
Huguguna nchi kavu, penye giza la ukiwa na uharibifu.
4Hung’oa mboga ya chumvi kwenye kichaka;
Na mizizi ya mretemu ni chakula chao.
5Hufukuzwa watoke kati ya watu;
Huwapigia kelele kama kumpigia mwivi.
6Lazima hukaa katika mianya ya mabonde,
Katika mashimo ya nchi na ya majabali.
7Hulia kama punda vichakani;
Hukusanyika chini ya upupu.
8Wao ni wana wa wapumbavu, naam, watoto wa wahuni;
Walifukuzwa kwa mijeledi watoke katika nchi.
9 # Ayu 17:6; Zab 35:15; 69:11 Na sasa mimi nimekuwa wimbo wao,
Naam, nimekuwa simo kwao.
10Wao hunichukia, na kujitenga nami,
Hawaachi kunitemea mate usoni.
11 # Ayu 12:18 Kwani ameilegeza kamba yake, na kunitesa,
Wala hawajizuii tena mbele yangu.
12 # Ayu 19:12 Kwa mkono wangu wa kuume huinuka kundi;
Huisukuma miguu yangu kando,
Na kunipandishia njia zao za uharibifu.
13 # Zab 69:26 Waiharibu njia yangu,
Wauzidisha msiba wangu,
Watu wasio na msaidizi.
14 # Zab 18:4; 69:14,15; Isa 8:7,8 Wanijilia kama wapitao katika ufa mpana;
Katikati ya magofu wanishambulia.
15Vitisho vimenigeukia;
Huifukuza heshima yangu kama upepo;
Na kufanikiwa kwangu kumepita kama wingu.
16 # 1 Sam 1:15; Isa 53:12; Zab 22:14; 42:4 Sasa nafsi yangu inamwagika ndani yangu;
Siku za mateso zimenishika.
17 # Ayu 33:19-21; Zab 6:2 Wakati wa usiku mifupa yangu huchomeka ndani yangu,
Na maumivu yanayonitafuna hayapumziki.
18 # Ayu 2:7 Kwa ugonjwa wangu kuwa na nguvu nyingi
Mavazi yangu yameharibika;
Hunikaza kama shingo ya kanzu yangu.
19Yeye amenibwaga topeni,
Nami nimekuwa kama mavumbi na majivu.
20 # Zab 22:2; Mt 15:23 Nakulilia wewe, wala huniitikii;
Nasimama, nawe wanitazama tu.
21Wewe umegeuka kuwa mkali kwangu;
Nawe waniudhi kwa uweza wa mkono wako.
22Waniinua juu hata upeponi, na kunipandisha juu yake;
Nawe waniyeyusha katika dhoruba.
23Kwani najua kuwa utanileta hata kifoni,
Niifikilie nyumba waliyoandikiwa wenye uhai wote.
24Je! Mtu katika kuanguka kwake hanyoshi mkono?
Na kulilia msaada katika msiba wake?
25 # Lk 19:41; Yn 11:35; Rum 12:15 Je! Mimi sikulia kwa ajili ya huyo aliyekuwa katika taabu?
Nafsi yangu, je! Haikusononeka kwa ajili ya wahitaji?
26 # Yer 8:15 Hapo nilipotazamia mema, ndipo yakaja mabaya;
Nami nilipongojea mwanga, likaja giza.
27Matumbo yangu yatokota, wala hayaachi;
Siku za taabu zimenijilia.
28 # Omb 3:1,2 Naenda nikiomboleza pasipo jua;
Nasimama katika mkutano, na kuulilia msaada.
29 # Zab 102:6 Mimi ni ndugu yao mbwa-mwitu,
Ni mwenzao mbuni.
30Ngozi yangu ni nyeusi, nayo yanitoka,
Na mifupa yangu imeteketea kwa hari.
31Kwa hiyo kinanda changu kimegeuzwa kuwa maombolezo,
Na filimbi yangu kuwa sauti yao waliao.

Iliyochaguliwa sasa

Ayu 30: SUV

Kuonyesha

Shirikisha

Nakili

None

Je, ungependa vivutio vyako vihifadhiwe kwenye vifaa vyako vyote? Jisajili au ingia