Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Ayu 13

13
1Tazama, jicho langu limeyaona hayo yote,
Sikio langu limeyasikia na kuelewa nayo.
2Hayo myajuayo ninyi, na mimi pia nayajua;
Mimi si duni kuliko ninyi.
3Hakika ningenena naye huyo Mwenyezi,
Nami nataka kuhojiana na Mungu.
4Lakini ninyi hubuni maneno ya uongo,
Ninyi nyote ni matabibu wasiofaa.
5 # Mit 17:28; Mhu 5:3; Amo 5:13; Yak 1:19 Laiti mngenyamaza kabisa!
Hilo lingekuwa hekima kwenu.
6Sikieni sasa basi hoja zangu,
Mkayasikie mashindano ya midomo yangu.
7 # Ayu 17:5; Rum 3:5,8 Je! Mtanena yasiyo ya haki kwa ajili ya Mungu,
Na kusema kwa udanganyifu kwa ajili yake?
8 # Mit 24:23 Je! Mtamwonyesha yeye upendeleo?
Mtamtetea Mungu?
9Je! Itafaa yeye kuwatafuta ninyi?
Au, kama kumdanganya mtu, je! Mtamdanganya yeye?
10Hakika atawakemea ninyi,
Mkiwapendelea watu kwa siri.
11Je! Huo ukuu wake hautawatia hofu,
Na utisho wake hautawaangukia?
12Matamko yenu ya hekima ni mithali ya majivu,
Ngome zenu ni ngome za udongo.
13Nyamazeni, niacheni, ili nipate kunena,
Na hayo yatakayonijilia na yaje.
14 # Zab 119:109 Nitaitwaa nyama ya mwili wangu katika meno yangu,
Na kuutwaa uhai wangu mkononi mwangu!
15 # Zab 23:4; Mit 14:32; Rum 8:38,39; Ayu 27:5 Tazama, ataniua; sina tumaini;#13:15 Au, ajaponiua, nitamngojea vivyo.
Ila hata hivyo nitaithibitisha njia yangu mbele yake.
16 # Isa 12:1,2 Hili nalo litakuwa ni wokovu wangu;
Kwani asiyemcha Mungu hatakaribia mbele yake.
17Sikieni sana maneno yangu,
Maelezo yangu na yaingie masikioni mwenu.
18Angalieni sasa, nimekwisha kulitengeneza neno langu,
Najua ya kuwa ni mwenye haki mimi.
19 # Ayu 33:6; Isa 50:8 Yuko nani atakayeshindana nami?
Maana sasa nitanyamaa kimya na kutoa roho.
Ayubu atoa Ombi la Kukata Tamaa
20Lakini msinifanyie mambo mawili, hayo tu,
Ndipo nami sitajificha usoni pako;
21Uondoe mkono wako usinilemee;
Na utisho wako usinitie hofu.
22Basi uite wakati huo, nami nitaitika;
Au, niache ninene mimi, nawe unijibu.
23Maovu yangu na dhambi zangu ni ngapi?
Nijulishe kosa langu na dhambi yangu.
24 # Zab 10:1; Isa 8:17; Omb 2:5; 2 The 3:15 Mbona umeuficha uso wako,
Na kunihesabu kuwa ni adui yako?
25 # Isa 17:13; 42:3 Je! Utalitaabisha jani lipeperushwalo?
Au, je! Utayafuatia hayo mabua makavu?
26 # Zab 25:7 Kwani umeandika maneno ya uchungu juu yangu,
Na kunirithisha maovu ya ujana wangu;
27 # Ayu 33:11 Waitia miguu yangu katika mkatale, na kuyaaua mapito yangu yote;
Wajiandikia alama kuzizunguka nyayo za miguu yangu;
28Nijapokuwa ni kama kitu kilichooza, kinachosinyaa,
Mfano wa nguo iliyoliwa na nondo.

Iliyochaguliwa sasa

Ayu 13: SUV

Kuonyesha

Shirikisha

Nakili

None

Je, ungependa vivutio vyako vihifadhiwe kwenye vifaa vyako vyote? Jisajili au ingia