Ayu 10
10
Nayachukia Maisha Yangu
1Nafsi yangu inachoka na maisha yangu;
Sitajizuia na kuugua kwangu;
Nitanena kwa uchungu wa roho yangu.
2Nitamwambia Mungu, Usinihukumie makosa;
Nionyeshe sababu ya wewe kushindana nami.
3Je! Ni vema kwako wewe kuonea,
Na kuidharau kazi ya mikono yako,
Na kuyaangazia mashauri ya waovu?
4 #
1 Sam 16:7; Lk 16:15; Ufu 1:14 Je! Wewe una macho ya kimwili,
Au je! Waona kama aonavyo binadamu?
5Je! Siku zako ni kama siku za mtu,
Au je! Miaka yako ni kama siku za mtu,
6Hata ukauliza-uliza habari za uovu wangu,
Na kuitafuta dhambi yangu,
7Ujapojua ya kuwa mimi si mwovu;
Wala hapana awezaye kuokoa na mkono wako?
8 #
Zab 119:73; Isa 43:7 Mikono yako imeniumba na kunifinyanga;
Nawe utageuka na kuniangamiza?
9 #
Mwa 2:7; Isa 45:9 Kumbuka, nakusihi ulivyonifinyanga kama vile udongo;
Nawe, je! Utanirudisha uvumbini tena?
10 #
Zab 139:14
Je! Wewe hukunimimina kama maziwa,
Na kunigandisha mfano wa jibini?
11Umenivika ngozi na nyama,
Na kuniunga pamoja kwa mifupa na mishipa.
12Umenijazi uhai na upendeleo,
Na maangalizi yako yameilinda roho yangu.
13Lakini mambo haya uliyaficha moyoni mwako;
Najua kuwa haya yamo nafsini mwako;
14Nikifanya dhambi, ndipo waniangalia,
Wala hutaniachilia na uovu wangu.
15 #
Zab 9:17; Isa 3:11; Mal 3:18; Ayu 9:12; Kut 3:7; Zab 25:18; Omb 1:20 Mimi nikiwa mbaya, ole wangu!
Nami nikiwa mwenye haki, walakini sitainua kichwa changu;
Mimi nimejaa aibu
Na kuyaangalia mateso yangu.
16 #
Isa 38:13; Omb 3:10 Kichwa changu kikijiinua, waniwinda kama simba;
Tena wajionyesha kwangu kuwa wa ajabu.
17Wewe warejeza upya hao mashahidi yako juu yangu,
Na kasirani yako waiongeza juu yangu;
Jeshi kwa jeshi juu yangu.
18Kwa nini basi kunitoa tumboni?
Ningekata roho, lisinione jicho lo lote.
19Ningalikuwa kama mtu asiyekuwapo;
Ningalichukuliwa kaburini kutoka tumboni.
20 #
Zab 39:13; Ayu 7:16 Je! Siku zangu si chache? Acha basi,
Usinisumbue, nipate ngaa kutuzwa moyo kidogo.
21 #
Ayu 3:5; Zab 88:12; 23:4 Kabla sijaenda huko ambako sitarudi kutoka huko tena,
Ni hiyo nchi ya giza, giza tupu;
22Ni nchi ya giza kuu, kama giza lenyewe lilivyo;
Ni nchi ya giza tupu, isiyo na matengezo ya mambo yo yote,
Nchi ambayo nuru yake ni kama giza.
Iliyochaguliwa sasa
Ayu 10: SUV
Kuonyesha
Shirikisha
Nakili
Je, ungependa vivutio vyako vihifadhiwe kwenye vifaa vyako vyote? Jisajili au ingia
Swahili Union Version (SUV): © Bible Society of Tanzania and Bible Society of Kenya, 1952, 1997. All rights reserved. lt/pgt ltpgtSwahili Union Version (SUV): Hakimiliki -1952, 1997: kwa: Chama cha Biblia cha Tanzania na Chama cha Biblia cha Kenya. Haki zote zimehifadhiwa.