Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Yer 39

39
Kuanguka kwa Yerusalemu
1 # 2 Fal 25:1-4; Yer 52:4-7 Hata ikawa, Yerusalemu ulipotwaliwa, (katika mwaka wa kenda wa Sedekia, mfalme wa Yuda, katika mwezi wa kumi, Nebukadreza, mfalme wa Babeli, na jeshi lake lote, wakaja juu ya Yerusalemu, wakauhusuru; 2katika mwaka wa kumi na mmoja wa Sedekia, mwezi wa nne, siku ya kenda ya mwezi, sehemu ya ukuta wa mji ilibomolewa;) 3wakuu wote wa mfalme wa Babeli wakaingia, wakaketi katika lango la katikati, yaani, Nergal-Shareza, mnyweshaji, Nebu-Sarseki, mkuu wa matowashi, Nergal-Shareza, mkuu wa wanajimu,#39:3 Au hivi, Nergal-Shareza, na Samgar-nebo, na Sarseki, na Rab-sarisi, na Nergal-Shareza, na Rab-magi. pamoja na wakuu wengine wote wa mfalme wa Babeli. 4Ikawa Sedekia, mfalme wa Yuda, na watu wote wa vita walipowaona, ndipo wakakimbia, wakatoka mjini usiku, kwa njia ya bustani ya mfalme, kwa lango lililokuwa kati ya zile kuta mbili; naye akatoka kwa njia ya Araba.#39:4Araba maana yake ni lile Bonde la mto wa Yordani na Bahari ya Chumvi. 5#Yos 5:10; Yer 32:4; 38:18; 2 Fal 23:33; Yer 52:9,26,27Lakini jeshi la Wakaldayo wakawafuatia, wakampata Sedekia katika nchi tambarare ya Yeriko; nao walipomkamata, wakamleta kwa Nebukadreza, mfalme wa Babeli, huko Ribla katika nchi ya Hamathi, naye akatoa hukumu juu yake. 6Ndipo mfalme wa Babeli akawaua wana wa Sedekia huko Ribla mbele ya macho yake; pia mfalme wa Babeli akawaua wakuu wote wa Yuda. 7#2 Fal 25:7; Eze 12:13; Yer 32:4; 52:11Pamoja na hayo akampofusha macho Sedekia, akamfunga kwa pingu ili amchukue mpaka Babeli. 8#2 Fal 25:9; 2 Nya 36:19; Isa 5:9; Yer 38:18Nao Wakaldayo wakaiteketeza nyumba ya mfalme, na nyumba za watu kwa moto, wakazibomoa kuta za Yerusalemu.
9 # 2 Fal 25:11; Yer 52:15 Basi, Nebuzaradani, amiri wa askari walinzi, akawachukua mateka mabaki ya watu waliosalia katika mji mpaka Babeli, na hao pia waliouacha mji na kujiunga naye, na mabaki ya watu waliosalia. 10Lakini Nebuzaradani, amiri wa askari walinzi, akawaacha baadhi ya maskini wa watu, waliokuwa hawana kitu, katika nchi ya Yuda, akawapa mashamba ya mizabibu na makonde wakati uo huo.
Yeremia Aachiliwa na Kumkumbuka Ebedmeleki
11Basi Nebukadreza, mfalme wa Babeli, akamwagiza Nebuzaradani, amiri wa askari walinzi, katika habari za Yeremia, akisema, 12Mtwae, umtunze sana, wala usimtende neno baya lo lote; lakini umtendee kama atakavyokuambia. 13Basi Nebuzaradani, amiri wa askari walinzi, na Nebu-Shazbani, mkuu wa matowashi, na Nergal-Shareza, mkuu wa wanajimu,#39:13 Au, Nebu-Shazbani, na Rab-sarisi, na Nergal-Shareza, na Rab-magi. na maakida wakuu wote wa mfalme wa Babeli, 14#Yer 38:28; 40:5; 26:24wakatuma watu wakamwondoa Yeremia katika uwanda wa walinzi, wakamweka katika mikono ya Gedalia, mwana wa Ahikamu, mwana wa Shafani, ili ampeleke nyumbani kwake; basi akakaa pamoja na hao watu.
15Basi neno la BWANA likamjia Yeremia, wakati ule alipokuwa amefungwa katika uwanda wa walinzi, kusema, 16#Mt 10:42; Dan 9:12Haya! Enenda ukaseme na Ebedmeleki, Mkushi, kusema, BWANA wa majeshi, Mungu wa Israeli, asema hivi, Tazama, nitaupatiliza mji huu maneno yangu kwa mabaya, wala si kwa mema; nayo yatatimizwa mbele yako katika siku hiyo. 17Lakini nitakuokoa wewe katika siku hiyo, asema BWANA; wala hutatiwa katika mikono ya watu wale unaowaogopa. 18#Yer 21:9; Rut 2:12; 1 Nya 5:20; Zab 32:7Kwa maana ni yakini, nitakuokoa, wala hutaanguka kwa upanga, lakini nafsi yako itakuwa kama nyara kwako; kwa kuwa ulinitumaini mimi, asema BWANA.

Iliyochaguliwa sasa

Yer 39: SUV

Kuonyesha

Shirikisha

Nakili

None

Je, ungependa vivutio vyako vihifadhiwe kwenye vifaa vyako vyote? Jisajili au ingia

YouVersion hutumia vidakuzi kubinafsisha matumizi yako. Kwa kutumia tovuti yetu, unakubali matumizi yetu ya vidakuzi kama ilivyoelezwa katika Sera yetu ya Faragha