Isa 21
21
Utabiri juu ya Babeli, Edomu na Arabuni
1 #
Zek 9:14
Ufunuo juu ya bara ya bahari. Kama tufani za Negebu#21:1Negebu tafsiri yake ni Nchi za kusini. zikaribiavyo kwa kasi, inakuja kutoka bara, toka nchi itishayo. 2#1 Sam 24:13; Yer 49:34; Isa 24:16; 13:17Nimeonyeshwa maono magumu; atendaye hila anatenda hila, mharibu anaharibu. Panda juu, Ee Elamu; husuru, Ee Umedi; mimi ninakomesha maombolezo yake yote. 3Kwa sababu hiyo viuno vyangu vimejaa maumivu, utungu umenishika, kama utungu wa mwanamke azaaye; ninaumwa sana, nisiweze kusikia; nimefadhaishwa wa hofu, nisiweze kuona. 4#Kum 28:67Moyo wangu unapiga-piga, utisho umenitaabisha, gizagiza la jioni nilipendalo limegeuka likanitetemesha. 5#Dan 5:5Wanaandika meza, wanaweka ulinzi, wanakula, wanakunywa. Simameni, enyi wakuu, itieni ngao mafuta. 6Maana Bwana ameniambia hivi, Enenda, weka mlinzi; aonayo na ayatangaze. 7Naye akiona kundi la wapanda farasi, wakienda wawili wawili, na kundi la punda, na kundi la ngamia; asikilize sana, akijitahidi kusikiliza. 8#Hab 2:1Ndipo akalia kama simba, Ee Bwana, mimi nasimama daima juu ya mnara wakati wa mchana, na kila usiku ninakaa katika zamu ya ulinzi wangu. 9#Isa 13:19; Yer 50:2; Ufu 14:8; 18:2Na, tazama, linakuja kundi la watu, wapanda farasi, wakienda wawili wawili. Akajibu na kusema, Babeli umeanguka, umeanguka; na sanamu zote za miungu yake zimevunjwa chini. 10#Yer 51:33; Mik 4:13; Hab 3:12Ewe niliyekufikicha, na nafaka ya sakafu yangu; Hayo niliyoyasikia kwa BWANA wa majeshi, Mungu wa Israeli, nimewapasha habari zake.
11 #
1 Nya 1:30; Eze 35:2; Oba 1:1 Ufunuo juu ya Duma. Mtu ananililia toka Seiri, Ee mlinzi, habari gani za usiku? Ee mlinzi, habari gani za usiku? 12Mlinzi akasema, Mchana unakuja na usiku pia; mkitaka kuuliza, ulizeni; njoni tena.
13 #
1 Nya 1:9
Ufunuo juu ya Arabuni.
Ndani ya msitu wa Arabuni mtalala,
Enyi misafara ya Wadedani.
14 #
Ayu 6:19
Waleteeni wenye kiu maji,
Enyi wenyeji wa nchi ya Tema;
Nendeni kuwalaki wakimbiao na chakula chao.
15Kwa maana wanakimbia mbele ya panga,
Upanga uliofutwa, na upinde uliopindwa,
Na mbele ya ukali wa vita.
16 #
Mwa 25:13; Zab 120:5; Wim 1:5; Isa 60:7 Kwa sababu Bwana ameniambia hivi, Katika muda wa mwaka, kama miaka ya mtu mwenye kuajiriwa, utaangamia utukufu wote wa Kedari. 17#Hes 23:19; 1 Sam 15:29; Isa 1:20; Mt 24:35; Mk 13:31; Lk 21:33; 1 Pet 1:25Na mabaki ya hesabu ya wavuta pinde, hao mashujaa wa Kedari watakuwa wachache; maana BWANA, Mungu wa Israeli, amenena neno hili.
Iliyochaguliwa sasa
Isa 21: SUV
Kuonyesha
Shirikisha
Nakili
Je, ungependa vivutio vyako vihifadhiwe kwenye vifaa vyako vyote? Jisajili au ingia
Swahili Union Version (SUV): © Bible Society of Tanzania and Bible Society of Kenya, 1952, 1997. All rights reserved. lt/pgt ltpgtSwahili Union Version (SUV): Hakimiliki -1952, 1997: kwa: Chama cha Biblia cha Tanzania na Chama cha Biblia cha Kenya. Haki zote zimehifadhiwa.