Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Isa 18

18
Utabiri juu ya Kushi
1 # Sef 2:12 Ole wa nchi ya uvumi wa mabawa,
Iliyoko mbali kupita mito ya Kushi;
2Ipelekayo wajumbe wake kwa njia ya bahari,
Na katika vyombo vya manyasi juu ya maji.
Nendeni, wajumbe wepesi, kwa watu warefu, laini;
Watu watishao tangu mwanzo wao hata sasa;
Taifa la wenye nguvu, wakanyagao watu,
Ambao mito inakata nchi yao.
3Enyi watu mkaao katika ulimwengu wote, na wenyeji wa dunia, bendera ikiinuliwa milimani, angalieni; na wakipiga tarumbeta, sikieni. 4Maana BWANA ameniambia hivi, Mimi nitatulia, na kuangalia katika makazi yangu, kama wakati wa mwangaza mweupe wa jua kali, mfano wa wingu la umande katika hari ya mavuno. 5Maana kabla ya mavuno, maua yaangukapo, na maua yakawa zabibu zianzazo kuiva, ndipo atakapoyakata matawi kwa miundu, na kuviondoa vitawi vilivyopanuka na kuvikata. 6Wote pamoja wataachiwa ndege wakali wa milimani, na hayawani wa nchi; ndege wakali watakaa juu yao wakati wa jua, na hayawani wote wa nchi watakaa juu yao wakati wa baridi. 7#Zab 68:31; Sef 3:10; Mal 1:11Wakati huo BWANA wa majeshi ataletewa hedaya na watu warefu, laini;
Watu watishao tangu mwanzo wao hata sasa;
Taifa la wenye nguvu, wakanyagao watu,
Ambao mito inakata nchi yao;
Mpaka mahali pa jina la BWANA wa majeshi, mlima Sayuni.

Iliyochaguliwa sasa

Isa 18: SUV

Kuonyesha

Shirikisha

Nakili

None

Je, ungependa vivutio vyako vihifadhiwe kwenye vifaa vyako vyote? Jisajili au ingia