Isa 10:20-25
Isa 10:20-25 SUV
Tena itakuwa katika siku hiyo mabaki ya Israeli, na hao waliopona wa nyumba ya Yakobo, hawatamtegemea tena yeye aliyewapiga, bali watamtegemea BWANA, Mtakatifu wa Israeli, kwa kweli. Mabaki, nao ni mabaki ya Yakobo, watamrudia Mungu, aliye mwenye nguvu. Maana watu wako, Ee Israeli, wajapokuwa wengi kama mchanga wa pwani, ni mabaki tu watakaorudi; kuangamiza kumekusudiwa, kunakofurika kwa haki. Kwa maana Bwana, BWANA wa majeshi, atayatimiza maangamizo yaliyokusudiwa katika nchi yote. Kwa hiyo Bwana, BWANA wa majeshi, asema hivi, Enyi watu wangu mkaao katika Sayuni, msiogope Ashuru, ingawa akupiga kwa fimbo, na kuliinua gongo lake juu yako, kwa namna ya Kimisri. Maana bado kitambo kidogo tu ghadhabu itakoma, na hasira yangu itageukia kuwaangamiza.