Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Ebr 4:1-3

Ebr 4:1-3 SUV

Basi, ikiwa ikaliko ahadi ya kuingia katika raha yake, na tuogope, mmoja wenu asije akaonekana ameikosa. Maana ni kweli, sisi nasi tumehubiriwa habari njema vile vile kama hao. Lakini neno lile lililosikiwa halikuwafaa hao, kwa sababu halikuchanganyika na imani ndani yao waliosikia. Maana sisi tulioamini tunaingia katika raha ile; kama vile alivyosema, Kama nilivyoapa kwa hasira yangu, Hawataingia rahani mwangu: ijapokuwa zile kazi zilimalizika tangu kuwekwa misingi ya ulimwengu.

Mipango ya Kusoma Bila Malipo na Ibada zinazohusiana na Ebr 4:1-3