Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Mwa 38:1-10

Mwa 38:1-10 SUV

Ikawa wakati ule, Yuda akashuka kutoka kwa ndugu zake, akamfikia mtu Mwadulami, jina lake Hira. Yuda akaona huko binti wa mtu Mkanaani, jina lake Shua. Akamtwaa, akaingia kwake. Naye akapata mimba, akazaa mwana, akamwita jina lake Eri. Akapata mimba tena, akazaa mwana, akamwita jina lake Onani. Akaendelea, akazaa tena mwana mwingine, akamwita jina lake Shela. Naye Yuda alikuwako huko Kezibu, alipomzaa. Yuda akamwoza mke Eri, mzaliwa wake wa kwanza, na jina lake huyo mke ni Tamari. Naye Eri, mzaliwa wa kwanza wa Yuda, alikuwa mbaya machoni pa BWANA; na BWANA akamwua. Yuda akamwambia Onani, Uingie kwa mke wa nduguyo, ukamwoe, ukamwinulie nduguyo uzao. Onani alijua ya kwamba huo uzao hautakuwa wake, ikawa, alipoingia kwa mke wa nduguye, akamwagia chini asimpe nduguye uzao. Neno hili alilolifanya likawa baya machoni pa BWANA, basi akamwua yeye naye.

Mipango ya Kusoma Bila Malipo na Ibada zinazohusiana na Mwa 38:1-10