Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Mwa 30:14-21

Mwa 30:14-21 SUV

Reubeni akaenda siku za mavuno ya ngano akaona tunguja kondeni, akazileta kwa Lea mamaye. Ndipo Raheli akamwambia Lea, Nipe mimi baadhi ya tunguja za mwanao. Naye akamwambia, Je! Ni jambo dogo kuninyang’anya mume wangu; hata wataka kuzitwaa tunguja za mwanangu pia? Raheli akamwambia, Kwa hiyo atalala kwako usiku huu kwa tunguja za mwanao. Yakobo akaja kutoka kondeni jioni, Lea akatoka kumlaki, akasema, Lazima uje kwangu, kwa sababu nimekuajiri, kwa tunguja za mwanangu; akalala kwake usiku ule. Mungu akamsikia Lea, naye akapata mimba, akamzalia Yakobo mwana wa tano. Lea akasema, Mungu amenipa ujira wangu, kwa sababu nimempa mume wangu mjakazi wangu. Akamwita jina lake Isakari. Lea akapata mimba tena, akamzalia Yakobo mwana wa sita. Lea akasema, Mungu amenipa mahari njema, sasa mume wangu atakaa nami, kwa kuwa nimemzalia wana sita. Akamwita jina lake Zabuloni. Baadaye akazaa binti, akamwita jina lake Dina.

Mipango ya Kusoma Bila Malipo na Ibada zinazohusiana na Mwa 30:14-21