BWANA akamwambia Musa, Nitafanya na neno hili ulilolinena, kwa maana umepata neema mbele zangu, nami nakujua jina lako. Akasema, Nakusihi unionyeshe utukufu wako. Akasema, Nitapitisha wema wangu wote mbele yako, nami nitalitangaza jina la BWANA mbele yako; nami nitamfadhili yeye nitakayemfadhili; nitamrehemu yeye nitakayemrehemu. Kisha akasema, Huwezi kuniona uso wangu, maana mwanadamu hataniona akaishi. BWANA akasema, Tazama, hapa pana mahali karibu nami, nawe utasimama juu ya mwamba; kisha itakuwa wakati unapopita utukufu wangu, nitakutia katika ufa wa ule mwamba, na kukufunika kwa mkono wangu hata nitakapokuwa nimekwisha kupita; nami nitaondoa mkono wangu, nawe utaniona nyuma yangu, bali uso wangu hautaonekana.
Soma Kut 33
Shirikisha
Linganisha Matoleo Yote: Kut 33:17-23
Hifadhi mistari, soma bila mtandao, tazama klipu za mafunzo, na zaidi!
YouVersion hutumia vidakuzi kubinafsisha matumizi yako. Kwa kutumia tovuti yetu, unakubali matumizi yetu ya vidakuzi kama ilivyoelezwa katika Sera yetu ya Faragha
Nyumbani
Biblia
Mipango
Video