Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Dan UTANGULIZI

UTANGULIZI
Danieli maana yake NI “Mungu ni Mwamuzi wangu”. Danieli ni mmoja wa vijana wa Yuda ambao Mfalme Nebukadneza wa II alipeleka uhamishoni Babeli. Huu ni uhamisho wa kwanza uliofanywa mwishoni mwa karne ya saba Kabla ya Kristo Kuzaliwa (1:1-6).
Mfalme Nebukadneza wa II alikuwa na shule nchini mwake. Shule hizo zilitoa elimu ya kusoma, kuandika, hesabu, lugha ya Kibabeli, elimu ya hekima, madawa, utabibu, theolojia, sheria, sanaa, elimu ya nyota na ustadi wa mazingaombwe. Mateka walioletwa Babeli walielimishwa ili wawe watumishi wao bora. Danieli na vijana wenzake walipewa elimu katika shule hizo. Danieli akawezeshwa na Mungu kuwa stadi wa maono na kutafsiri ndoto (11:21; 5:30). Baadaye alichaguliwa kuwa kiongozi mkuu wa serikali (kama Yusufu alivyokuwa Misri) (2:47-48; 5:25-28; 6:25-27).
Wayahudi waliguswa sana na imani yao walipochukuliwa utumwani. Mji mtakatifu Yerusalemu na nchi yao ya ahadi vilipoharibiwa walijawa na maswali mengi kuhusu agano lao na Mungu pamoja na ulinzi wake. Ujumbe wa Danieli ulikuwa wa kulaumu ukaidi na kiburi cha wafalme wa Babeli na kuwataka watubu (4:19, 25, 27). Watawala wote na mamlaka zao ziko chini ya enzi ya Mungu. Uwezo na nguvu za watu vinaweza kujaribu kushindana na Mungu lakini huishia kwenye kushindwa. Mamlaka ya Mungu ni kubwa kuliko uwezo wa watu. Kama ilivyo katika ujumbe wa nabii Isaya sehemu ya pili, Yeremia na Ezekieli, Danieli alisisitiza uvumilivu, uaminifu na imani thabiti kwa Mungu na matumaini. Yeye mwenyewe ni kielelezo chao cha kumtegemea Mungu. Danieli alikuwa mtu wa sala, maombezi na kufunga (2:17-23; 6:10; 9:1-23; 10:2-3,11). Aliwapa watu matumaini kuwa Mungu ataangamiza watesaji wao. Pia alisema kuwa Wayahudi watakuwa huru, salama na uonevu utakoma.
Yaliyomo:
1. Masimulizi yahusuyo Danieli na wenzake, Sura 1–6
2. Maono ya Danieli, Sura 7–12

Iliyochaguliwa sasa

Dan UTANGULIZI: SUV

Kuonyesha

Shirikisha

Nakili

None

Je, ungependa vivutio vyako vihifadhiwe kwenye vifaa vyako vyote? Jisajili au ingia

YouVersion hutumia vidakuzi kubinafsisha matumizi yako. Kwa kutumia tovuti yetu, unakubali matumizi yetu ya vidakuzi kama ilivyoelezwa katika Sera yetu ya Faragha