2 Sam 22
22
Wimbo wa Shukrani wa Daudi
1 #
Kut 15:1
Basi Daudi akamwambia BWANA maneno ya wimbo huu, siku ile BWANA alipomwokoa mikononi mwa adui zake zote, na mkononi mwa Sauli; 2#Mwa 15:1; Kum 32:4; 1 Sam 2:2; Zab 18:2; 91:2; Mit 18:10; Mt 18:11akasema,
BWANA ndiye jabali langu, na ngome yangu, na mwokozi wangu,
naam, wangu;
3 #
Ebr 2:13; Mwa 15:1; Zab 3:3; Mit 30:5; Lk 1:69; Mit 18:10; Zab 9:9; 18:2; Isa 32:2; Isa 32:2; Yer 16:19 Mungu wa mwamba wangu, nitamwamini yeye;
Ngao yangu, na pembe ya wokovu wangu, mnara wangu, na
makimbilio yangu;
Mwokozi wangu, waniokoa na jeuri.
4Nitamwita BWANA astahiliye kusifiwa;
Hivyo nitaokoka na adui zangu.
5Maana mawimbi ya mauti yalinizunguka,
Mafuriko ya uovu yakanitia hofu.
6Kamba za kuzimu zilinizunguka;
Mitego ya mauti ikanikabili.
7 #
Zab 116:4; Yon 2:2; Kut 3:7 Katika shida yangu nalimwita BWANA,
Naam, nikamlalamikia Mungu wangu;
Naye akaisikia sauti yangu hekaluni mwake,
Kilio changu kikaingia masikioni mwake.
8 #
Amu 5:4; Ayu 26:11; Zab 18:7; 77:18 Ndipo nchi ilipotikisika na kutetemeka,
Misingi ya mbinguni ikasuka-suka
Na kutikisika, kwa sababu alikuwa na ghadhabu.
9 #
Zab 97:3; Hab 3:5; Ebr 12:29 Kukapanda moshi kutoka puani mwake,
Moto ukatoka kinywani mwake ukala;
Makaa yakawashwa nao.
10 #
Isa 64:1
Aliziinamisha mbingu akashuka;
Kukawa na giza kuu chini ya miguu yake.
11 #
Zab 104:3
Akapanda juu ya kerubi akaruka;
Naam, alionekana juu ya mabawa ya upepo.
12Akafanya giza hema zake za kumzunguka,
Makusanyiko ya maji, mawingu makuu ya mbinguni.
13Toka mwangaza uliokuwa mbele zake
Makaa ya moto yakawashwa.
14 #
Isa 30:30
BWANA alipiga radi toka mbinguni,
Naye Aliye juu akaitoa sauti yake.
15 #
Kum 32:23; Zab 7:13; 77:17; Hab 3:11 Akapiga mishale, akawatawanya;
Umeme, naye akawatapanya.
16Ndipo ilipoonekana mikondo ya bahari,
Misingi ya ulimwengu ikafichuliwa,
Kwa kukemea kwake BWANA,
Kwa mvumo wa pumzi ya puani mwake.
17Alipeleka kutoka juu, akanishika;
Akanitoa katika maji mengi;
18Akaniokoa na adui yangu mwenye nguvu,
Na wale walionichukia;
Maana walikuwa na nguvu kuliko mimi.
19Walinikabili siku ya msiba wangu;
Lakini BWANA alikuwa tegemeo langu.
20 #
Zab 31:8; 2 Sam 15:26 Akanitoa akanipeleka panapo nafasi;
Aliniponya kwa kuwa alipendezwa nami.
21BWANA alinitendea sawasawa na haki yangu;
Sawasawa na usafi wa mikono yangu akanilipa.
22Maana nimezishika njia za BWANA,
Wala sikumwasi Mungu wangu.
23 #
Kum 7:12
Maana hukumu zake zote zilikuwa mbele yangu;
Na kwa habari za amri zake, sikuziacha.
24 #
Mwa 6:9; Ayu 1:1; Yn 1:47 Nami nalikuwa mkamilifu kwake,
Nikajilinda na uovu wangu.
25Basi BWANA amenilipa sawasawa na haki yangu;
Sawasawa na usafi wa mikono yangu mbele zake.
26 #
Mt 5:7
Kwa mtu mwenye fadhili utakuwa mwenye fadhili
Kwa mkamilifu utajionyesha kuwa mkamilifu;
27 #
Law 26:23
Kwake ajitakasaye utajionyesha kuwa mtakatifu;
Na kwa mpotovu utajionyesha kuwa mkaidi.
28 #
Kut 3:7; Zab 12:5; Mt 5:3 Na watu wanaoonewa wewe utawaokoa;
Ila macho yako ni juu ya wenye kiburi, uwadhili.
29Kwa kuwa wewe u taa yangu, Ee BWANA;
Na BWANA ataniangazia giza langu.
30Maana kwa msaada wako nafuatia jeshi;
Kwa msaada wa Mungu wangu naruka ukuta.
31 #
Kum 32:4; Dan 4:37; Ufu 15:3; Zab 12:6; Mit 30:5 Mungu njia yake ni kamilifu;
Ahadi ya BWANA imehakikishwa;
Yeye ndiye ngao yao
Wote wanaomkimbilia.
32 #
Kum 32:31; 1 Sam 2:2; Isa 45:5,6 Maana ni nani aliye Mungu, ila BWANA?
Ni nani aliye mwamba, ila Mungu wetu?
33 #
Zab 27:1; Kum 18:13 Mungu ndiye ngome yangu yenye nguvu;
Naye huwaongoza wakamilifu katika njia yake.
34 #
Hab 3:19
Huifanya miguu yangu kuwa kama ya kulungu;
Na kunisimamisha mahali pangu pa juu.
35Ananifundisha mikono yangu vita;
Hata mikono yangu yaupinda upinde wa shaba.
36Nawe umenipa ngao ya wokovu wako;
Na unyenyekevu wako umenikuza.
37Umezifanyizia nafasi hatua zangu,
Wala miguu yangu haikuteleza.
38Nimewafuatia adui zangu, na kuwaangamiza;
Wala sikurudi nyuma hata walipokomeshwa.
39Nami nimewakomesha na kuwapiga-piga wasiweze kusimama;
Naam, wameanguka chini ya miguu yangu.
40Maana umenifunga mshipi wa nguvu kwa vita;
Umenitiishia chini yangu walioniondokea.
41Naam, adui zangu umewafanya wanipe visogo,
Ili niwakatilie mbali wanaonichukia.
42 #
1 Sam 28:6; Ayu 27:9; Mit 1:28 Walitazama, lakini hakuna wa kuokoa;
Walimwita BWANA, lakini hakuwajibu.
43Ndipo nikawaponda kama mavumbi ya nchi,
Nikawakanyaga kama matope ya njiani, nikawatawanya.
44 #
Kum 28:13; Isa 55:5 Nawe umeniokoa na mashindano ya watu wangu;
Umenihifadhi niwe kichwa cha mataifa;
Watu nisiowajua watanitumikia.
45Wageni watanijia wakinyenyekea;
Kwa kusikia tu habari zangu,
Mara watanitii.
46 #
Mik 7:17
Wageni nao watatepetea,
Watatoka katika ngome zao wakitetemeka.
47 #
Zab 89:26
BWANA ndiye aliye hai;
Na ahimidiwe mwamba wangu;
Na atukuzwe Mungu wa mwamba wa wokovu wangu;
48 #
Zab 144:2
Naam, Mungu anipatiaye kisasi,
Na kuwatweza watu chini yangu,
49Na kunileta nje nitoke kwa adui zangu;
Naam, waniinua juu yao walioniinukia;
Waniponya na mtu wa jeuri.
50 #
Rum 15:9
Basi, BWANA, nitakushukuru kati ya mataifa,
Nami nitaliimbia jina lako.
51Ampa mfalme wake wokovu mkuu;
Amfanyia fadhili masihi#22:51 Au, mtiwa mafuta (taz. 1 Sam. 2:10). wake,
Daudi na mzao wake, hata milele.
Iliyochaguliwa sasa
2 Sam 22: SUV
Kuonyesha
Shirikisha
Nakili
Je, ungependa vivutio vyako vihifadhiwe kwenye vifaa vyako vyote? Jisajili au ingia
Swahili Union Version (SUV): © Bible Society of Tanzania and Bible Society of Kenya, 1952, 1997. All rights reserved. lt/pgt ltpgtSwahili Union Version (SUV): Hakimiliki -1952, 1997: kwa: Chama cha Biblia cha Tanzania na Chama cha Biblia cha Kenya. Haki zote zimehifadhiwa.