Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

2 Fal 6:1-6

2 Fal 6:1-6 SUV

Kisha, wana wa manabii wakamwambia Elisha, Angalia basi, mahali tukaapo mbele yako ni padogo kwetu. Basi twende mpaka Yordani, twakuomba, tutwae huko kila mtu mti mmoja, ili tujifanyie huko mahali pa kukaa. Akajibu, Haya! Nendeni. Mmoja wao akasema, Uwe radhi, basi nakusihi, uende pamoja na watumishi wako. Akajibu, Nitakwenda. Basi, akaenda pamoja nao. Nao walipofika Yordani, wakakata miti. Lakini mmojawapo alipokuwa katika kukata boriti, chuma cha shoka kikaanguka majini; akalia, akasema, Ole wangu! Bwana wangu, kwani kiliazimiwa kile. Mtu wa Mungu akasema, Kilianguka wapi? Akamwonyesha mahali. Akakata kijiti, akakitupa pale pale, chuma kikaelea.

Soma 2 Fal 6

Mipango ya Kusoma Bila Malipo na Ibada zinazohusiana na 2 Fal 6:1-6