Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

2 Nya 4

4
Mapambo ya Hekalu
1 # Kut 27:1; 1 Fal 9:25; 2 Fal 16:14; Eze 43:13 Tena akafanya madhabahu ya shaba, mikono ishirini urefu wake, na mikono ishirini upana wake, na mikono kumi kwenda juu kwake. 2#Kut 30:18; 1 Fal 7:23Tena akaifanya bahari ya kusubu, mikono kumi toka ukingo hata ukingo, ya mviringo, na kwenda juu kwake ilikuwa mikono mitano; na uzi wa mikono thelathini kuizunguka kabisa. 3#1 Fal 7:24Na chini yake palikuwa na mifano ya ng’ombe,#4:3 Au, maboga (1 Wafalme 7:24). walioizunguka pande zote, kwa mikono kumi, wakiizunguka pande zote ile bahari. Ng’ombe walikuwa safu mbili, wakayeyushwa hapo ilipoyeyushwa hiyo bahari. 4Ikakaa juu ya ng’ombe kumi na wawili, watatu wakitazama kaskazini, na watatu wakitazama magharibi, na watatu wakitazama kusini, na watatu wakitazama mashariki; na bahari iliwekwa juu yao, na pande zao za nyuma zote zilikuwa ndani. 5#1 Fal 7:26Na unene wake ulikuwa nyanda nne, na ukingo wake ukafanywa kama ukingo wa kikombe, kama ua la yungi; huingia bathi elfu tatu, kukaa ndani yake. 6#1 Fal 7:38; Ebr 9:9Akafanya na birika kumi, akaziweka tano upande wa kuume, na tano upande wa kushoto, za kuoshea; ndizo walizooshea mambo ya kafara; lakini hiyo bahari ilikuwa ya makuhani ya kuogea. 7#1 Fal 7:49; Kut 25:31Akavifanya vinara vya taa kumi vya dhahabu, kadiri ya vilivyoagiziwa; akavitia hekaluni, vitano upande wa kuume, na vitano upande wa kushoto. 8#1 Fal 7:48Akafanya na meza kumi, akazitia hekaluni, tano upande wa kuume, na tano upande wa kushoto. Kisha akafanya mabakuli mia ya dhahabu. 9#1 Fal 6:36Tena akaufanya ua wa makuhani, na ua mkubwa, nayo milango yake, akaifunikiza kwa shaba milango yake. 10#1 Fal 7:39Nayo bahari akaiweka upande wa kuume kwa mashariki, kuelekea kusini. 11#1 Fal 7:40Na Huramu akayafanya masufuria, na majembe, na mabakuli.
Basi Huramu akamaliza kufanya hiyo kazi, aliyomfanyia mfalme Sulemani ya nyumba ya Mungu; 12#1 Fal 7:41zile nguzo mbili, na vimbe, na taji mbili zilizokuwa juu ya nguzo; nazo nyavu mbili za kuzifunika vimbe mbili za taji zilizokuwa juu ya nguzo; 13#Kut 28:33,34; 1 Fal 7:20; Wim 4:13; Yer 52:23na makomamanga mia nne ya nyavu mbili; safu mbili za makomamanga kwa kila wavu, kuzifunika vimbe mbili za taji zilizokuwa juu ya nguzo. 14#1 Fal 7:27,43Akayafanya na matako, na mabirika akafanya juu ya matako; 15bahari moja, na ng’ombe kumi na wawili chini yake. 16#1 Fal 7:14,45Masufuria pia, na majembe, na nyuma, na vyombo vyake vyote, Huramu#4:16 Au, Huramu babaye. akamfanyia mfalme Sulemani kwa nyumba ya BWANA, vya shaba iliyokatuka. 17#1 Fal 7:46Katika uwanda wa Yordani ndipo mfalme alipovisubu, katika udongo mzito kati ya Sukothi na Sereda. 18#1 Fal 7:47Ndivyo alivyovifanya Sulemani vyombo hivyo vyote, vingi sana; kwa kuwa uzani wa shaba ulikuwa hautafutikani. 19#1 Fal 7:48-50; 2 Fal 24:13; Yer 28:3; Dan 5:2,3; Kut 25:30; 1 Nya 28:16Basi Sulemani akavifanya vyombo vyote vilivyokuwamo nyumbani mwa Mungu, madhabahu ya dhahabu pia, nazo meza, ambazo juu yake iliwekwa mikate ya wonyesho; 20#Kut 27:20,21na vinara na taa zake, ziwake kama ilivyoagizwa mbele ya chumba cha ndani, vya dhahabu iliyosafika; 21#Kut 25:31; 37:20; 1 Fal 6:18-35na maua, na taa, na makoleo, ya dhahabu, ndiyo dhahabu bora; 22#1 Fal 6:31na mikasi, na mabakuli, na miiko, na vyetezo, vya dhahabu iliyosafika; na kwa habari za mahali pa kuingia nyumbani, milango yake ya ndani ya patakatifu pa patakatifu, na milango ya nyumba, yaani ya hekalu, ilikuwa ya dhahabu.

Iliyochaguliwa sasa

2 Nya 4: SUV

Kuonyesha

Shirikisha

Nakili

None

Je, ungependa vivutio vyako vihifadhiwe kwenye vifaa vyako vyote? Jisajili au ingia