Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

2 Nya 35

35
Pasaka Yaadhimishwa
1 # 2 Fal 23:21; Kut 12:6; Hes 9:3; Ezr 6:19; Eze 45:21 Naye Yosia akamfanyia BWANA pasaka huko Yerusalemu; wakachinja pasaka siku ya kumi na nne ya mwezi wa kwanza. 2#2 Nya 23:18; Ezr 6:18; 1 Nya 22:19; 2 Nya 29:5,11Akawasimamisha makuhani katika malinzi yao, akawatia moyo kufanya utumishi wa nyumba ya BWANA. 3#Kum 33:10; 2 Nya 30:22; 34:14; Mal 2:7; 2 Nya 5:7; 1 Nya 23:26Akawaambia Walawi, waliowafundisha Israeli wote, waliotakasika kwa BWANA, Wekeni sanduku takatifu katika nyumba aliyoijenga Sulemani, mwana wa Daudi, mfalme wa Israeli; hamtakuwa tena na mzigo mabegani; sasa mtumikieni BWANA, Mungu wenu, na watu wake Israeli. 4#1 Nya 9:10; 23:1; 24:1; 2 Nya 8:14Mkajiweke tayari kwa kadiri ya nyumba za baba zenu, kwa zamu zenu, kama alivyoandika Daudi mfalme wa Israeli, na kama alivyoandika Sulemani mwanawe. 5#Zab 134:1Mkasimame katika patakatifu, kama walivyogawanyika ndugu zenu, wana wa watu, kufuata nyumba za mababa, kadiri ya mgawanyiko wa kila nyumba ya baba, ya Walawi. 6#Kut 19:10; 2 Nya 29:5; 30:3,15; Ezr 6:20; Ayu 1:5; Zab 51:7; Yoe 2:16; Ebr 9:13,14Mkachinje pasaka, mkajitakase, mkawatengenezee ndugu zenu, kutenda sawasawa na neno la BWANA kwa mkono wa Musa. 7#Mik 6:7; 2 Nya 30:24Tena Yosia akawapa wana wa watu, matoleo ya makundi, wana-kondoo na wana-mbuzi, yote yawe kwa ajili ya matoleo ya pasaka, wote waliokuwako, wakipata thelathini elfu, na ng’ombe elfu tatu; hao walitoka katika mali za mfalme. 8#2 Kor 9:7Na wakuu wake wakawapa watu, na makuhani na Walawi matoleo ya hiari. Hilkia na wana na Yehieli, wakubwa wa nyumba ya Mungu, wakawapa makuhani, kuwa matoleo ya pasaka, wana-kondoo elfu mbili na mia sita, na ng’ombe mia tatu. 9Konania naye, na Shemaya, na Nethaneli, ndugu zake, na Hashabia, na Yeieli, na Yozabadi, wakuu wa Walawi, wakawapa Walawi, kuwa matoleo ya pasaka, wana-kondoo elfu tano, na ng’ombe mia tano. 10#Ezr 6:18Hivyo huduma ikatengenezwa, wakasimama makuhani mahali pao, na Walawi kwa zamu zao, kama alivyoamuru mfalme. 11#Law 1:5,6; 2 Nya 29:22,34Wakachinja pasaka, nao makuhani wakamimina damu waliyopokea mikononi mwao, Walawi wakachuna. 12#Law 3:3Wakaziondoa sadaka za kuteketezwa, wawape wana wa watu, kama walivyogawanyika kufuata nyumba za mababa, ili wamtolee BWANA, kama ilivyoandikwa katika kitabu cha Musa. Nao ng’ombe wakawafanya vivyo hivyo. 13#Kut 12:8; Kum 16:7; 1 Sam 2:13-15Wakaioka moto pasaka kama ilivyo sheria; wakatokosa matoleo matakatifu vyunguni, na masufuriani, na makaangoni, wakawachukulia upesi wana wa watu wote. 14Baadaye wakajiandalia wenyewe, na makuhani; kwa sababu makuhani, wana wa Haruni, walikuwa na kazi ya kutoa sadaka za kuteketezwa, na mafuta hata usiku; kwa hiyo Walawi wakajiandalia wenyewe, na makuhani, wana wa Haruni. 15#1 Nya 25:1; 9:17,18; 26:14Nao waimbaji, wana wa Asafu wakasimama mahali pao, kama alivyoamuru Daudi, na Asafu, na Hemani, na Yeduthuni mwonaji wa mfalme; nao mabawabu walikuwa katika kila lango; hawakuhitaji kuondoka katika huduma yao, kwa kuwa ndugu zao Walawi wakawaandalia. 16Basi huduma yote ya BWANA ikatengenezwa siku ile ile, kuifanya pasaka, na kutoa sadaka za kuteketezwa juu ya madhabahu ya BWANA, kama alivyoamuru mfalme Yosia. 17#Kut 12:15; 13:6; Law 23:5,8; Hes 28:16,17; Kum 16:3-8; 2 Nya 30:21; 1 Kor 5:7,8Wana wa Israeli waliokuwapo wakafanya pasaka wakati ule, na sikukuu ya mikate isiyochachwa muda wa siku saba. 18#2 Fal 23:22,23Wala haikufanyika pasaka kama ile katika Israeli tangu siku za nabii Samweli; wala wafalme wa Israeli hawakufanya hata mmoja wao pasaka kama ile Yosia aliyoifanya, pamoja na makuhani, na Walawi, na Yuda wote na Israeli waliokuwapo, na wenyeji wa Yerusalemu. 19Katika mwaka wa kumi na nane wa kutawala kwake Yosia ikafanyika pasaka hiyo.
Kushinda kwa Farao Neko na Kifo cha Yosia
20 # 2 Fal 23:29; Yer 46:2 Baada ya hayo yote, alipokwisha Yosia kulitengeneza hekalu, Neko, mfalme wa Misri, akakwea ili kupigana Karkemishi karibu na Frati; naye Yosia akatoka juu yake. 21#2 Fal 18:25; Isa 36:10; Dan 4:35Lakini yeye akatuma kwake wajumbe, kusema, Ni nini niliyo nayo mimi na wewe, Ee mfalme wa Yuda? Sikuja juu yako leo, lakini juu ya nyumba niliyo na vita nayo; naye Mungu ameniamuru nifanye haraka; acha basi kumpinga Mungu, aliye pamoja nami, asikuharibu. 22#1 Fal 14:2; 22:30; 2 Nya 18:29Walakini Yosia hakukubali kumgeuzia uso mbali, akajibadilisha apate kupigana naye, asiyasikilize maneno ya Neko, yaliyotoka kinywani kwa Mungu, akaja kupigana bondeni mwa Megido. 23#1 Fal 22:34Nao wapiga upinde wakampiga Yosia; naye mfalme akawaambia watumishi wake, Niondoeni; kwani nimejeruhiwa sana. 24#2 Fal 23:30; Zek 12:11Basi watumishi wake wakamtoa garini, wakamtia katika gari la pili alilokuwa nalo, wakamleta Yerusalemu; naye akafa, akazikwa makaburini mwa babaze. Wakamlilia Yosia Yuda wote na Yerusalemu. 25#Yer 22:10; Omb 4:20; Mhu 12:5; Yer 9:17; Amo 5:16; Mt 9:23; Yer 22:20Naye Yeremia akamlilia Yosia; na waimbaji wote waume kwa wake wakamtaja Yosia katika maombolezo yao, hata leo; hata wakayafanya kuwa ada kwa Israeli; nayo, tazama, yameandikwa katika maombolezo. 26#Zab 112:6; Mit 10:7; 22:1Basi mambo yote ya Yosia yaliyosalia, na matendo yake mema, sawasawa na yote yaliyoandikwa katika torati ya BWANA, 27na mambo yake, ya kwanza na ya mwisho, tazama, yameandikwa katika kitabu cha wafalme wa Israeli na Yuda.

Iliyochaguliwa sasa

2 Nya 35: SUV

Kuonyesha

Shirikisha

Nakili

None

Je, ungependa vivutio vyako vihifadhiwe kwenye vifaa vyako vyote? Jisajili au ingia