Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

2 Nya 28

28
Utawala wa Ahazi
1 # 2 Fal 16:2 Ahazi alikuwa na umri wa miaka ishirini alipoanza kutawala; akatawala katika Yerusalemu miaka kumi na sita; wala hakufanya yaliyo ya adili machoni pa BWANA, kama Daudi babaye; 2#Kut 34:17; Law 19:4; Amu 2:11bali akaziendea njia za wafalme wa Israeli, akawafanyizia mabaali sanamu za kusubu. 3#2 Fal 23:10; Yer 7:31; Law 18:21; 2 Fal 16:3; 2 Nya 33:6; Eze 16:20; Mik 6:7Tena akafukiza uvumba katika bonde la mwana wa Hinomu, akawateketeza wanawe motoni, sawasawa na machukizo ya mataifa, aliowafukuza BWANA mbele ya wana wa Israeli. 4Akatoa dhabihu na kufukiza uvumba katika mahali pa juu, na vilimani, na chini ya kila mti wenye majani mabichi.
Shamu na Israeli Waishinda Yuda
5 # Isa 7:1; 2 Fal 16:5 Kwa hiyo BWANA, Mungu wake, akamtia mkononi mwa mfalme wa Shamu; wakampiga, wakachukua wa watu wake wafungwa wengi sana, wakawaleta Dameski. Tena akatiwa mkononi mwa mfalme wa Israeli, aliyempiga mapigo makuu. 6#2 Fal 15:27; Isa 9:21; Yos 23:16; Yer 2:19Kwa kuwa Peka mwana wa Remalia akawaua katika Yuda siku moja watu mia na ishirini elfu, mashujaa wote; kwa sababu walikuwa wamemwacha BWANA, Mungu wa baba zao. 7Naye Zikri, mtu hodari wa Efraimu, akawaua Maaseya mwana wa mfalme, na Azrikamu mkuu wa nyumba, na Elkana, aliyekuwa wa pili wake mfalme.
Obedi Aingilia Kati
8 # 2 Nya 11:4 Wana wa Israeli wakachukua wa ndugu zao wafungwa mia mbili elfu, wanawake, na wana, na binti, pia wakachukua kwao nyara nyingi, wakazileta nyara Samaria. 9#Amu 3:8; Zab 69:26; Isa 10:5; 47:6; Eze 25:12,15; 26:2; Oba 1:10; Zek 1:15; Mwa 4:10; 11:4; Ezr 9:6; Ufu 18:5Lakini kulikuwako huko nabii wa BWANA, jina lake aliitwa Odedi; akatoka kuwalaki jeshi waliokuja Samaria, akawaambia, Angalieni, kwa kuwa BWANA, Mungu wa baba zenu, aliwakasirikia Yuda, yeye amewatia mikononi mwenu, nanyi mmewaua kwa ghadhabu iliyofikia mbinguni. 10#Law 25:39; Yer 25:29; 1 Pet 4:17Na sasa mwanuia kuwatawala wana wa Yuda na Yerusalemu, wawe kwenu watumwa na wajakazi; lakini ninyi nanyi je! Hamna hatia zenu wenyewe juu ya BWANA, Mungu wenu? 11#Yak 2:13Haya, nisikieni mimi basi, mwarudishe wafungwa, mliowachukua mateka wa ndugu zenu; kwa maana ghadhabu ya BWANA iliyo kali i juu yenu. 12Ndipo wakaondoka juu ya hao waliotoka vitani baadhi ya wakuu wa wana wa Efraimu, Azaria, mwana wa Yohanani, na Berekia mwana wa Meshilemothi, na Yehizkia mwana wa Shalumu, na Amasa mwana wa Hadlai, 13#Hes 32:14; Yos 22:17wakawaambia, Hamtawaleta wafungwa humo; kwa sababu mnayanuia yatakayotutia hatiani mbele za BWANA, kuongeza dhambi zetu, na hatia yetu; maana hatia yetu ni kubwa, na ghadhabu kali ipo juu ya Israeli. 14Basi watu wenye silaha wakawaacha wafungwa na nyara mbele ya wakuu na kusanyiko lote. 15#2 Fal 6:22; Mt 25:21,22; Lk 6:27; Rum 12:20; Kum 34:3; Amu 1:16Wakaondoka wale watu waliotajwa majina yao, wakawatwaa wafungwa, wakawavika kwa zile nyara wote wao waliokuwa uchi, wakawapa mavazi na viatu, wakawalisha, wakawanywesha, wakawatia mafuta, wakawapandisha waliokuwa dhaifu miongoni mwao juu ya punda wakawaleta Yeriko, mji wa mitende, kwa ndugu zao; kisha wakarudi Samaria.
Ashuru Yakataa Kuisaidia Yuda
16 # 2 Fal 16:7; Isa 7:1-9 Wakati ule mfalme Ahazi akatuma wajumbe kwa mfalme wa Ashuru ili amsaidie. 17#Law 26:18Kwa kuwa Waedomi walikuwa wamekuja tena, na kuwapiga Yuda, na kuwachukua wafungwa. 18#Yos 15:22; Eze 16:27,57Wafilisti pia walikuwa wameingia miji ya Shefela, na ya Negebu ya Yuda, nao wameutwaa Beth-shemeshi, na Ayaloni, na Gederothi, na Soko pamoja na miji yake, na Timna pamoja na miji yake, na Gimzo pia na miji yake; wakakaa humo. 19#2 Nya 21:2; Kut 32:25; Ufu 3:17; 16:15Kwa maana BWANA aliinamisha Yuda kwa ajili ya Ahazi mfalme wa Israeli; kwa kuwa yeye aliwafanyia Yuda aibu, na kumwasi BWANA mno. 20#2 Fal 15:29; 16:7-9; Isa 7:20Na Tiglath-pileseri mfalme wa Ashuru akamjia, akamfadhaisha, asimtie nguvu kwa lo lote. 21Kwa maana Ahazi alitwaa sehemu katika nyumba ya BWANA, na katika nyumba ya mfalme, na ya wakuu, akampa mfalme wa Ashuru; asisaidiwe na jambo hilo.
Ukafiri na Kifo cha Ahazi
22 # 2 Nya 33:12; Zab 50:15; Isa 1:5; Yer 5:3; Hos 5:15; Ufu 16:11 Na wakati alipofadhaishwa, akazidi kumwasi BWANA, huyo mfalme Ahazi. 23#2 Nya 25:14; Yer 44:17,18Kwani akaitolea dhabihu miungu ya Dameski iliyompiga, akasema, Kwa sababu miungu ya wafalme wa Shamu imewasaidia wao, mimi nitaitolea dhabihu, ili inisaidie mimi. Lakini ndiyo iliyomwangamiza yeye na Israeli wote. 24#2 Nya 29:3,7Tena Ahazi akakusanya vyombo vyote vya nyumba ya Mungu, akavikata vipande vipande vyombo vya nyumba ya Mungu, akaifunga milango ya nyumba ya BWANA; akajifanyizia madhabahu katika kila pembe ya Yerusalemu. 25Na katika kila mji wa Yuda akafanya mahali pa juu pa kuifukizia miungu mingine uvumba, akamkasirisha BWANA, Mungu wa babaze. 26#2 Fal 16:19,20; 2 Nya 20:34; 27:7-9Basi mambo yake yote yaliyosalia, na njia zake zote, za kwanza na za mwisho, tazama, yameandikwa katika kitabu cha wafalme wa Yuda na Israeli. 27Ahazi akalala na babaze, wakamzika mjini, yaani, Yerusalemu; maana hawakumleta makaburini mwa wafalme wa Israeli; na Hezekia mwanawe akatawala mahali pake.

Iliyochaguliwa sasa

2 Nya 28: SUV

Kuonyesha

Shirikisha

Nakili

None

Je, ungependa vivutio vyako vihifadhiwe kwenye vifaa vyako vyote? Jisajili au ingia