Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

2 Nya 27

27
Utawala wa Yothamu
1 # 2 Fal 15:32; 1 Nya 3:12; Isa 1:1; Hos 1:1; Mik 1:1 Yothamu alikuwa na umri wa miaka ishirini na mitano alipoanza kutawala; akatawala katika Yerusalemu miaka kumi na sita; na jina la mamaye aliitwa Yerusha binti Sadoki. 2#2 Nya 26:16-21; Zab 119:120; 2 Fal 15:35Akafanya yaliyo ya adili machoni pa BWANA, sawasawa na yote aliyoyafanya Uzia babaye; isipokuwa hakuingia hekaluni mwa BWANA. Lakini watu walikuwa wakali kufanya maovu. 3#2 Nya 33:14; Neh 3:26Ndiye aliyelijenga lango la juu la nyumba ya BWANA, na juu ya ukuta wa Ofeli akajenga sana. 4Tena akajenga miji katika milima ya Yuda, na mwituni akajenga ngome na minara. 5#2 Nya 20:1; 26:8; 2 Fal 3:4; Yer 49:1-6Kisha akapigana na mfalme wa wana wa Amoni, akawashinda. Na wana wa Amoni wakampa mwaka ule ule talanta mia za fedha, na kori elfu kumi za ngano, na elfu kumi za shayiri. Hayo ndiyo waliyomtolea wana wa Amoni, mwaka wa pili pia, na mwaka wa tatu. 6#1 Sam 2:30; 1 Nya 12:14; 19:3; Zab 34:8; 40:4Basi Yothamu akawa na nguvu, kwa kuwa alizitengeneza njia zake mbele za BWANA, Mungu wake. 7Na mambo yote ya Yothamu yaliyosalia, na vita vyake vyote, na njia zake, tazama, yameandikwa katika kitabu cha wafalme wa Israeli na Yuda. 8Alikuwa na umri wa miaka ishirini na mitano alipoanza kutawala; akatawala miaka kumi na sita huko Yerusalemu. 9Yothamu akalala na babaze, wakamzika katika mji wa Daudi; na Ahazi mwanawe akatawala mahali pake.

Iliyochaguliwa sasa

2 Nya 27: SUV

Kuonyesha

Shirikisha

Nakili

None

Je, ungependa vivutio vyako vihifadhiwe kwenye vifaa vyako vyote? Jisajili au ingia