Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

2 Nya 19

19
1Yehoshafati mfalme wa Yuda akarudi Yerusalemu nyumbani kwake kwa amani. 2#1 Sam 9:9; Zab 15:4; Mit 1:10; 2 Nya 32:25Yehu mwana wa Hanani mwonaji akatoka kwenda kumlaki, akamwambia mfalme Yehoshafati, Je! Imekupasa kuwasaidia waovu, na kuwapenda wamchukiao BWANA? Kwa ajili ya hayo ghadhabu i juu yako itokayo kwa BWANA. 3#2 Nya 12:12; 30:19; Ezr 7:10Walakini yameonekana mema ndani yako, kwa kuwa umeyaondoa maashera katika nchi, na moyo wako umeukaza kumtafuta Mungu.
Matengenezo Aliyoyafanya Yehoshafati
4Na Yehoshafati akakaa Yerusalemu; akatoka tena kwenda kati ya watu toka Beer-sheba mpaka milima ya Efraimu, akawarudisha kwa BWANA, Mungu wa baba zao. 5#Kum 16:18Akasimamisha makadhi katika nchi, katikati ya miji yote yenye maboma ya Yuda, mji kwa mji; 6#Kum 1:17; Zab 82:1; Mhu 5:8akawaambia hao makadhi, Angalieni myafanyayo; kwa kuwa hammfanyii mwanadamu hukumu, ila BWANA; naye yupo pamoja nanyi katika neno la hukumu. 7#Kum 32:4; Rum 9:14; Kum 10:17; Ayu 34:19; Mdo 10:34; Rum 2:11; Gal 2:6; Efe 6:9; Kol 3:25; 1 Pet 1:17Basi sasa hofu ya BWANA na iwe juu yenu; angalieni mkaifanye; kwa maana kwa BWANA, Mungu wetu, hapana uovu, wala kujali nafsi za watu, wala kupokea zawadi. 8#Kum 16:18; 17:9-13; 1 Nya 23:4; 26:19; 2 Nya 17:8Tena katika Yerusalemu Yehoshafati akasimamisha wa Walawi na makuhani, na wakuu wa mbari za mababa wa Israeli wawe kwa hukumu ya BWANA, na kwa mateto. Nao wakarudi Yerusalemu. 9#2 Sam 23:3Akawaagiza, akasema, Ndivyo mtakavyotenda kwa hofu ya BWANA, kwa uaminifu, na kwa moyo kamili. 10#Kum 17:8; Hes 16:46; Eze 3:18Na kila mara watakapowajia na teto ndugu zenu wakaao mijini mwao, kati ya damu na damu, kati ya torati na amri, sheria na hukumu, mtawaonya, wasiingie hatiani mbele za BWANA, mkajiliwa na ghadhabu ninyi na ndugu zenu; fanyeni haya wala hamtakuwa na hatia. 11Tena angalieni, Amaria, kuhani mkuu, yu juu yenu kwa maneno yote ya BWANA; naye Zebadia, mwana wa Ishmaeli, jemadari wa nyumba ya Yuda, kwa maneno yote ya mfalme; Walawi nao watakuwa wasimamizi mbele yenu. Jitieni nguvu, mtende, naye BWANA awe pamoja nao walio wema.

Iliyochaguliwa sasa

2 Nya 19: SUV

Kuonyesha

Shirikisha

Nakili

None

Je, ungependa vivutio vyako vihifadhiwe kwenye vifaa vyako vyote? Jisajili au ingia

YouVersion hutumia vidakuzi kubinafsisha matumizi yako. Kwa kutumia tovuti yetu, unakubali matumizi yetu ya vidakuzi kama ilivyoelezwa katika Sera yetu ya Faragha