Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

2 Nya 17

17
Utawala wa Yehoshafati
1Na Yehoshafati mwanawe akatawala mahali pake, akajitia nguvu juu ya Israeli. 2#2 Nya 11:11; 15:8Akaweka jeshi katika miji yote yenye maboma ya Yuda, akatia na askari walinzi katika nchi ya Yuda, na katika miji ya Efraimu, aliyoitwaa Asa babaye. 3#Rum 8:31Naye BWANA alikuwa pamoja na Yehoshafati, kwa kuwa alikwenda katika njia za kwanza za Daudi babaye, asiyatafute mabaali; 4#Lk 1:6; 1 Fal 12:28lakini alimtafuta Mungu wa baba yake, akaenda katika amri zake, wala si katika matendo ya Israeli. 5#1 Sam 10:27; 1 Fal 10:25,27; 2 Nya 18:1Kwa hiyo BWANA akauthibitisha ufalme mkononi mwake; Yehoshafati akaletewa zawadi na Yuda wote; basi akawa na mali na heshima tele. 6#1 Fal 22:43; 2 Nya 14:3; 15:17; 19:3Ukainuliwa moyo wake katika njia za BWANA; na zaidi ya hayo akapaondoa mahali pa juu, na maashera, katika Yuda. 7#2 Nya 15:3Tena, katika mwaka wa tatu wa kutawala kwake, akawatuma wakuu wake, yaani, Ben-haili, na Obadia, na Zekaria, na Nethaneli, na Mikaya, ili kufundisha mijini mwa Yuda; 8na pamoja nao Walawi, yaani, Shemaya, na Nethania, na Zebadia, na Asaheli, na Shemiramothi, na Yehonathani, na Adonia, na Tobia, na Tob-adonia, Walawi; na pamoja nao Elishama na Yehoramu, makuhani. 9#2 Nya 35:3; Law 10:11; Neh 8:7; Mal 2:7Wakafundisha katika Yuda, wenye kitabu cha torati ya BWANA; wakazunguka katika miji yote ya Yuda, wakafundisha kati ya watu. 10#Mwa 35:5; Kut 15:15; Kum 11:25; 2 Nya 14:14Hofu ya BWANA ikaziangukia falme za nchi zote zilizozunguka Yuda, wasipigane vita na Yehoshafati. 11#2 Sam 8:2Na baadhi ya Wafilisti walimletea Yehoshafati zawadi, na fedha ya kodi; Waarabu nao wakamletea makundi, kondoo waume saba elfu na mia saba, na mabeberu saba elfu na mia saba. 12Ukuu wake Yehoshafati ukazidi sana; akajenga katika Yuda ngome na miji ya hazina. 13Naye alikuwa na kazi nyingi katika miji ya Yuda; na watu wa vita, watu mashujaa humo Yerusalemu. 14Na hivi ndivyo walivyohesabiwa kwa mbari za baba zao; wa Yuda, maakida wa maelfu; Adna jemadari, na pamoja naye watu mashujaa mia tatu elfu; 15na wa pili wake Yehohanani akida, na pamoja naye mia mbili na themanini elfu; 16#Amu 5:2,9; 1 Nya 29:9-17; Zab 110:3; 2 Kor 8:12na baada yake Amasia mwana wa Zikri, aliyejitoa kwa BWANA kwa moyo, na pamoja naye mia mbili elfu, watu mashujaa; 17na wa Benyamini; Eliada mtu shujaa, na pamoja naye mia mbili elfu wenye nyuta na ngao; 18na wa pili wake Yehozabadi, na pamoja naye mia na themanini elfu waliojiweka tayari kwa vita. 19Hao ndio waliomngojea mfalme, zaidi ya hao mfalme aliowaweka katika miji yenye maboma katika Yuda yote.

Iliyochaguliwa sasa

2 Nya 17: SUV

Kuonyesha

Shirikisha

Nakili

None

Je, ungependa vivutio vyako vihifadhiwe kwenye vifaa vyako vyote? Jisajili au ingia

YouVersion hutumia vidakuzi kubinafsisha matumizi yako. Kwa kutumia tovuti yetu, unakubali matumizi yetu ya vidakuzi kama ilivyoelezwa katika Sera yetu ya Faragha