Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

2 Nya 15

15
1 # Hes 24:2; Amu 3:10; 2 Sam 23:2; 2 Nya 20:14; 24:20; 2 Pet 1:21 Ndipo roho ya Mungu ikamjia Azaria mwana wa Odedi; 2#Yak 4:8; 1 Nya 28:9; 2 Nya 33:12,13; Yer 29:13; Mt 7:7; 2 Nya 12:1-3; 24:20; Rum 11:1,2; Ebr 12:25naye akatoka ili amlaki Asa, akamwambia, Nisikieni, Ee Asa, na Yuda wote na Benyamini; BWANA yu pamoja nanyi, mkiwa pamoja naye; nanyi mkimtafuta ataonekana kwenu; lakini mkimwacha atawaacha ninyi. 3#Hos 3:4; Law 10:11Basi tangu siku nyingi Israeli wamekuwa hawana Mungu wa kweli, wala hawana kuhani afundishaye, wala hawana torati; 4#Kum 4:29lakini walipomgeukia BWANA, Mungu wa Israeli, katika msiba wao, na kumtafuta, akaonekana kwao. 5#Amu 5:6Hata na zamani zile hakukuwa na amani kwake atokaye, wala kwake aingiaye, ila fadhaa kubwa juu yao wote wakaao katika nchi. 6#Mt 24:7Wakavunjika-vunjika, taifa juu ya taifa, na mji juu ya mji; kwani Mungu aliwafadhaisha kwa shida zote. 7#Mwa 15:1; Rut 2:12; Zab 58:11; Mt 5:12-46; Lk 6:35; Kol 3:24Nanyi jipeni nguvu, wala mikono yenu isilegee; kwa maana kazi yenu itakuwa na ijara. 8#2 Nya 13:19Naye Asa alipoyasikia maneno hayo, yaani, unabii wa mwana wa Odedi nabii, akatiwa nguvu, akayaondolea mbali machukizo yote katika nchi ya Yuda na Benyamini, na katika miji aliyoitwaa milimani mwa Efraimu; akaifanyiza tena madhabahu ya BWANA, iliyokuwako mbele ya ukumbi wa BWANA. 9#2 Nya 11:16Akakusanya Yuda wote na Benyamini, na hao wageni waliokaa kwao, wa Efraimu, na wa Manase, na wa Simeoni; kwa kuwa walimwangukia wengi katika Israeli, walipoona kwamba BWANA, Mungu wake, alikuwa pamoja naye. 10Basi wakakusanyika huko Yerusalemu mwezi wa tatu, katika mwaka wa kumi na tano wa kumiliki kwake Asa. 11#2 Nya 14:15Wakamchinjia BWANA siku ile, katika nyara walizozileta, dhabihu za ng’ombe mia saba, na kondoo elfu saba. 12#2 Fal 23:3; 2 Nya 34:31; Neh 10:29Wakafanya agano, ya kuwa watamtafuta BWANA, Mungu wa baba zao, kwa mioyo yao yote, na kwa roho zao zote; 13#Kut 22:20; Kum 13:5,9,15na ya kwamba ye yote asiyemtafuta BWANA, Mungu wa Israeli, atauawa, akiwa mdogo au mkubwa, kwamba ni mwanamume au mwanamke. 14Wakamwapia BWANA kwa sauti kuu, na kwa kelele, na kwa mapanda, na kwa baragumu. 15Na Yuda wote wakakifurahia kile kiapo; kwani wameapa kwa moyo wao wote, na kumtafuta kwa mapenzi yao pia; naye ameonekana kwao; naye BWANA akawastarehesha pande zote. 16#1 Fal 15:2,10Hata na Maaka mamaye Asa, mfalme akamwondolea daraja yake asiwe malkia, kwa kuwa amefanya sanamu ya kuchukiza kwa Ashera; basi Asa akaikata sanamu yake, akaiponda, akaiteketeza penye kijito cha Kidroni. 17#Kum 12:7; 1 Fal 3:2-4; 15:14; 2 Fal 12:3; 2 Nya 14:3,5Lakini mahali pa juu hapakuondolewa katika Israeli; ila moyo wake Asa ulikuwa mkamilifu siku zake zote. 18Akavileta nyumbani mwa Mungu vitu alivyovitakasa babaye, na vile alivyovitakasa mwenyewe, fedha, na dhahabu, na vyombo. 19Wala hapakuwa na vita tena hata mwaka wa thelathini na tano wa kutawala kwake Asa.

Iliyochaguliwa sasa

2 Nya 15: SUV

Kuonyesha

Shirikisha

Nakili

None

Je, ungependa vivutio vyako vihifadhiwe kwenye vifaa vyako vyote? Jisajili au ingia

YouVersion hutumia vidakuzi kubinafsisha matumizi yako. Kwa kutumia tovuti yetu, unakubali matumizi yetu ya vidakuzi kama ilivyoelezwa katika Sera yetu ya Faragha