1 Fal 16
16
1 #
1 Fal 21:20-24; 2 Nya 19:2; 20:24 Ndipo neno la BWANA likamjia Yehu mwana wa Hanani juu ya Baasha, kusema, 2#1 Fal 14:7; 1 Sam 2:8; 15:17; Zab 75:6,7; Yer 27:5; Dan 2:21; 4:17; 1 Fal 15:34Kwa kuwa mimi nilikuinua kutoka katika mavumbi, na kukufanya uwe mkuu juu ya watu wangu Israeli; nawe umeiendea njia ya Yeroboamu, na kuwakosesha watu wangu Israeli, hata wanighadhibishe kwa makosa yao; 3#1 Fal 14:10; 15:29; 21:22-24; Isa 66:24angalia, kuondoa nitawaondoa Baasha na jamaa yake; tena nitaifanya nyumba yako iwe kama nyumba ya Yeroboamu mwana wa Nebati. 4#1 Fal 14:11Mtu amfiaye Baasha mjini mbwa watamla; naye amfiaye mashambani ndege wa angani watamla. 5#2 Nya 16:1Basi, mambo yote ya Baasha yaliyosalia, na aliyoyafanya, na nguvu zake, je! Hayakuandikwa katika kitabu-cha-tarehe cha wafalme wa Israeli? 6#1 Fal 14:11; 15:21Baasha akalala na babaze, akazikwa katika Tirza; naye Ela mwanawe akatawala mahali pake. 7#Zab 115:4; Isa 2:8; 44:9; 1 Fal 14:14; 15:27; 2 Fal 10:30,31; Hos 1:4Tena neno la BWANA likaja kwa mkono wa nabii Yehu mwana wa Hanani juu ya Baasha, na juu ya nyumba yake, kwa sababu ya mabaya yote aliyoyatenda machoni pa BWANA, akimghadhibisha kwa kazi ya mikono yake, kwa kufanana na nyumba ya Yeroboamu, na kwa sababu aliiharibu.
Ela Atawala Israeli
8Katika mwaka wa ishirini na sita wa Asa mfalme wa Yuda, Ela mwana wa Baasha alianza kutawala juu ya Israeli huko Tirza, akatawala miaka miwili. 9#1 Fal 15:27; 2 Fal 9:31; 12:20; 15:10,25,30; 1 Sam 25:36-38; 2 Sam 13:28,29; 1 Fal 20:16; Ayu 31:3; Mit 20:1; Isa 1:28Na mtumwa wake Zimri, jemadari wa nusu ya magari yake, akamfanyia fitina; alipokuwako Tirza akinywa hata kulewa nyumbani mwa Arsa, aliyekuwa juu ya nyumba huko Tirza; 10Zimri akaingia akampiga, akamwua, katika mwaka wa ishirini na saba wa Asa mfalme wa Yuda, akatawala mahali pake. 11#1 Sam 25:24Ikawa, alipoanza kutawala, mara alipoketi juu ya kiti chake cha enzi, akawaua nyumba yote ya Baasha; hakumwachia mwanamume ye yote, wa jamaa zake, wala wa rafiki zake. 12#Isa 40:8; 1 Pet 1:25Hivyo Zimri akaiharibu nyumba yote ya Baasha, sawasawa na neno la BWANA, alilolinena juu ya Baasha kwa Yehu nabii, 13#Isa 3:16; Kum 32:21; 1 Sam 12:21; 2 Fal 17:15; Isa 41:29; Yer 10:8,15; Yon 2:8; 1 Kor 8:4; 10:19kwa sababu ya makosa yake Baasha, na makosa yote ya Ela mwanawe, waliyoyakosa, na kuwakosesha Israeli, wakimghadhibisha BWANA, Mungu wa Israeli, kwa matendo yao ya ubatili. 14Na mambo yote ya Ela yaliyosalia, na yote aliyoyafanya, je! Hayakuandikwa katika kitabu-cha-tarehe cha wafalme wa Israeli?
Zimri Atawala Israeli
15 #
Ayu 20:5; Zab 37:35; 1 Fal 15:27 Katika mwaka wa ishirini na saba wa Asa mfalme wa Yuda, Zimri akatawala muda wa siku saba huko Tirza. Basi, watu walikuwa wametua maragoni kupigana na Gibethoni, ulio wa Wafilisti. 16Na hao watu waliokuwako maragoni wakasikia habari ya kwamba Zimri amefanya fitina, tena amempiga mfalme; kwa hiyo Israeli wote wakamfanya Omri, jemadari wa jeshi, awe mfalme juu ya Israeli siku ile maragoni. 17Omri akapanda kutoka Gibethoni, na Israeli wote pamoja naye, wakauhusuru Tirza. 18#Amu 9:54Ikawa Zimri alipoona ya kuwa mji umetwaliwa, akaingia ngomeni mwa nyumba ya mfalme, akaiteketeza nyumba ya mfalme juu yake kwa moto, akafa; 19#Zab 9:16; 1 Fal 12:28; 15:26kwa sababu ya makosa aliyoyakosa, akifanya mabaya machoni pa BWANA, kwa kuiendea njia ya Yeroboamu na makosa yake aliyoyafanya akiwakosesha Israeli. 20Na mambo yote ya Zimri yaliyosalia na fitina yake aliyoifanya, je! Hayakuandikwa katika kitabu-cha-tarehe cha wafalme wa Israeli?
Omri Atawala Israeli
21 #
Isa 9:18
Ndipo watu wa Israeli wakatengwa sehemu mbili; nusu ya watu wakamfuata Tibni mwana wa Ginathi, ili wamfanye mfalme; nusu wakamfuata Omri. 22Lakini hao watu waliomfuata Omri wakawashinda watu waliomfuata Tibni mwana wa Ginathi; basi akafa Tibni, akatawala Omri. 23Katika mwaka wa thelathini na moja wa Asa, mfalme wa Yuda, Omri alianza kutawala juu ya Israeli, akatawala miaka kumi na miwili. Akatawala huko Tirza miaka sita.
Samaria Kuwa Mji Mkuu Mpya
24 #
1 Fal 13:32; 2 Fal 17:24; Yn 4:4 Kisha akanunua kilima cha Samaria kwa Shemeri kwa talanta mbili za fedha; akajenga juu ya kilima kile, akauita mji alioujenga Samaria, kwa kuliandama jina lake Shemeri, aliyekuwa mwenye kilima. 25#1 Fal 14:9; Mik 6:16Omri akafanya yaliyo mabaya machoni pa BWANA, akatenda maovu kuliko wote waliomtangulia; 26#Yer 16:19; Mdo 14:15; Rum 1:21kwa kuwa aliiendea njia yote ya Yeroboamu mwana wa Nebati, na makosa yake, aliyowakosesha Israeli, ili kumghadhibisha BWANA, Mungu wa Israeli, kwa matendo yao ya ubatili. 27Nayo mambo yote ya Omri yaliyosalia aliyoyatenda, na uthabiti alioufanya, je! Hayakuandikwa katika kitabu-cha-tarehe cha wafalme wa Israeli? 28Omri akalala na babaze, akazikwa huko Samaria; na Ahabu mwanawe akatawala mahali pake.
Ahabu Atawala Israeli
29Ahabu mwana wa Omri alianza kutawala juu ya Israeli katika mwaka wa thelathini na nane wa Asa mfalme wa Yuda; akatawala Ahabu mwana wa Omri juu ya Israeli katika Samaria miaka ishirini na miwili. 30Ahabu mwana wa Omri akafanya yaliyo mabaya machoni pa BWANA kuliko wote waliomtangulia.
Ahabu Amwoa Yezebeli na Kuabudu Baali
31 #
Mwa 6:2; Kum 7:3; Yos 23:12; 1 Fal 18:4-19; 19:1,2; 2 Fal 9:30-37; Amu 18:7; 1 Fal 21:25; 2 Fal 10:18; 17:16 Ikawa, kama ingalikuwa neno dogo tu kuyaendea makosa ya Yeroboamu mwana wa Nebati, akamwoa Yezebeli binti Ethbaali, mfalme wa Wasidoni, akaenda akamtumikia Baali, akamsujudia. 32#2 Fal 10:21-27Akamjengea Baali madhabahu katika nyumba ya Baali, aliyoijenga huko Samaria. 33#Kut 34:13; 2 Fal 17:10; Yer 17:2; 1 Fal 21:25Ahabu akaifanya Ashera; Ahabu akazidi kumghadhibisha BWANA, Mungu wa Israeli, kuliko wafalme wote wa Israeli waliomtangulia.
34 #
Hes 15:30; Yos 6:26; Zab 119:89,126; Mit 13:13; Isa 40:8; Mt 24:35; Mk 13:31; Lk 21:33; 1 Pet 1:25 Katika siku zake, Hieli Mbetheli akajenga Yeriko; akatia misingi yake kwa kufiwa na Abiramu mzaliwa wake wa kwanza, na kuyaweka malango yake kwa kufiwa na mwana wake mdogo Segubu; sawasawa na neno la BWANA alilolinena kwa Yoshua mwana wa Nuni.
Iliyochaguliwa sasa
1 Fal 16: SUV
Kuonyesha
Shirikisha
Nakili
Je, ungependa vivutio vyako vihifadhiwe kwenye vifaa vyako vyote? Jisajili au ingia
Swahili Union Version (SUV): © Bible Society of Tanzania and Bible Society of Kenya, 1952, 1997. All rights reserved. lt/pgt ltpgtSwahili Union Version (SUV): Hakimiliki -1952, 1997: kwa: Chama cha Biblia cha Tanzania na Chama cha Biblia cha Kenya. Haki zote zimehifadhiwa.