Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

1 Fal 15

15
Abijamu Atawala Yuda: Kuabudu Sanamu na Vita
1Mwaka wa kumi na nane wa mfalme Yeroboamu mwana wa Nebati, Abiya alianza kutawala juu ya Yuda. 2#2 Nya 11:21; 13:2Miaka mitatu akatawala huko Yerusalemu; na jina la mamaye aliitwa Maaka, binti Absalomu. 3#1 Fal 11:4; Zab 119:80Akaziendea dhambi zote za babaye, alizozifanya kabla yake; wala moyo wake haukuwa mkamilifu na BWANA, Mungu wake, kama moyo wa Daudi babaye. 4#Mwa 12:2; 19:29; 2 Nya 21:7; Isa 37:35Walakini kwa ajili ya Daudi, BWANA, Mungu wake, akampa taa humo Yerusalemu, amwinue mwanawe baada yake, na kuufanya imara Yerusalemu; 5#1 Fal 14:8; Lk 1:6kwa sababu Daudi alifanya yaliyo mema machoni pa BWANA, wala hakukosa katika yote aliyomwamuru, siku zote za maisha yake, isipokuwa katika habari ya Uria, Mhiti.
6Basi kulikuwa na vita kati ya Rehoboamu#15:6 Au, Abiya. na Yeroboamu siku zote za maisha yake. 7#2 Nya 13:2,3,22Na mambo yote ya Abiya yaliyosalia, na yote aliyoyafanya, je! Hayakuandikwa katika kitabu-cha-tarehe cha wafalme wa Yuda? Kulikuwa na vita kati ya Abiya na Yeroboamu. 8#2 Nya 14:1Abiya akalala na baba zake, wakamzika mjini mwa Daudi. Akatawala Asa mwanawe mahali pake.
Asa Atawala Yuda
9Mwaka wa ishirini wa Yeroboamu mfalme wa Israeli, Asa alianza kutawala juu ya Yuda. 10Akatawala miaka arobaini na mmoja huko Yerusalemu; na jina la mamaye aliitwa Maaka, binti Absalomu. 11#2 Nya 14:2; 15:17Basi, Asa akafanya yaliyo mema machoni pa Mungu, kama alivyofanya babaye Daudi. 12#1 Fal 14:21; 22:46Akawafukuza mahanithi katika nchi, akaziondoa sanamu zote walizozifanya baba zake. 13#Kum 13:6; 33:9; 2 Nya 15:16; Mt 10:37; 19:29; Lk 12:51,53; 14:26; Kut 32:20Hata na Maaka, mamaye, akamwondolea daraja yake asiwe malkia, kwa kuwa amefanya sanamu ya kuchukiza kwa Ashera; basi Asa akaikata sanamu yake akaiteketeza penye kijito cha Kidroni. 14#1 Fal 22:43; 2 Nya 15:17Lakini mahali pa juu hapakuondoshwa; ila moyo wake Asa ulikuwa mkamilifu kwa BWANA siku zake zote. 15Akavileta vile vitu alivyovitakasa baba yake, na vile alivyovitakasa yeye mwenyewe, katika nyumba ya BWANA, fedha; na dhahabu, na vyombo.
Ushirikiano na Shamu dhidi ya Israeli
16Kulikuwa na vita kati ya Asa na Baasha mfalme wa Israeli siku zao zote. 17#2 Nya 16:1; Yos 18:25; 1 Sam 15:34; 1 Fal 12:27Kisha, Baasha mfalme wa Israeli akaondoka juu ya Yuda, akaujenga Rama, ili asimwache mtu ye yote kutoka wala kuingia kwa Asa mfalme wa Yuda. 18#1 Fal 20:1-5,33,34; 2 Fal 8:7-15; 2 Nya 16:2; Mwa 14:15; 1 Fal 11:23Ndipo Asa akazitwaa fedha zote na dhahabu zilizosalia katika hazina za nyumba ya BWANA, na hazina za nyumba ya mfalme, akazitia mikononi mwa watumishi wake; mfalme Asa akawatuma kwa Ben-hadadi, mwana wa Tabrimoni, mwana wa Hezioni, mfalme wa Shamu, aliyekaa Dameski, akasema, 19Tumepatana mimi nawe, na baba yangu na baba yako; angalia, nimekuletea zawadi, fedha na dhahabu; basi nenda, uyavunje mapatano yako na Baasha mfalme wa Israeli, ili aniondokee mimi. 20#2 Fal 15:29; Amu 18:29; 2 Sam 20:14Naye Ben-hadadi akamsikiliza mfalme Asa, akawatuma wakuu wa majeshi yake juu ya miji ya Israeli, akapiga Iyoni, na Dani, na Abel-beth-maaka na Kinerothi yote, na nchi yote ya Naftali. 21Ikawa Baasha aliposikia habari hiyo akaacha kuujenga Rama, akaenda akakaa Tirza. 22#2 Nya 16:6; 1 Sam 8:16,17; Yos 21:17; 1 Sam 7:6Ndipo mfalme Asa akatangaza kwa Yuda pia; asiachiliwe mtu; nao wakayachukua mawe ya Rama na miti yake, aliyoijengea Baasha; naye mfalme Asa akajenga kwa vitu hivyo Geba wa Benyamini na Mispa.
23 # 2 Nya 16:12; Zab 90:10; Mhu 12:1 Na mambo yote ya Asa yaliyosalia, na nguvu zake zote, na yote aliyoyafanya, na miji aliyoijenga, je! Hayakuandikwa katika kitabu-cha-tarehe cha wafalme wa Yuda? Lakini alipokuwa mzee alikuwa na ugonjwa wa miguu. 24#1 Fal 22:41-43; 2 Nya 17:1; Mt 1:8Asa akalala na babaze, akazikwa pamoja na babaze mjini mwa Daudi baba yake. Na Yehoshafati mwanawe akatawala mahali pake.
Nadabu Atawala Israeli
25Nadabu mwana wa Yeroboamu alianza kutawala juu ya Israeli, mwaka wa pili wa Asa mfalme wa Yuda, akatawala juu ya Israeli miaka miwili. 26#1 Fal 12:30Akafanya yaliyo mabaya machoni pa BWANA, akaiendea njia ya baba yake, na kosa lake alilowakosesha Israeli.
27 # 1 Fal 14:14; Yos 19:44; 21:23; 1 Fal 16:15 Basi Baasha wa Ahiya, wa mbari ya Isakari, akamfanyia fitina; Baasha akampiga huko Gibethoni ulio wa Wafilisti; kwani Nadabu na Israeli wote walikuwa wakiuhusuru Gibethoni. 28#Kum 32:35Mwaka wa tatu wa Asa mfalme wa Yuda Baasha akamwua, akatawala mahali pake. 29#1 Fal 14:10,14; Ayu 18:13-21; Zab 21:10; 37:28,38; Isa 14:20Ikawa mara alipotawala, akawapiga nyumba yote ya Yeroboamu. Hakumwachia Yeroboamu mwenye pumzi ye yote, hata alipomharibu sawasawa na neno la BWANA alilolinena kwa mtumishi wake Ahiya, Mshiloni; 30kwa sababu ya makosa yake Yeroboamu aliyoyakosa, ambayo kwa hayo aliwakosesha Israeli; kwa sababu ya chukizo lake alilomchukiza BWANA, Mungu wa Israeli, hata kumghadhibisha. 31Basi mambo yote ya Nadabu yaliyosalia, na yote aliyoyafanya, je! Hayakuandikwa katika kitabu-cha-tarehe cha wafalme wa Israeli? 32Kulikuwa na vita kati ya Asa na Baasha mfalme wa Israeli siku zao zote.
Baasha Atawala Israeli
33Katika mwaka wa tatu wa Asa mfalme wa Yuda, Baasha mwana wa Ahiya alianza kutawala juu ya Israeli wote huko Tirza, akatawala miaka ishirini na minne. 34#1 Fal 12:28,29; 13:33; 14:16Akafanya yaliyo mabaya machoni pa BWANA akaiendea njia ya Yeroboamu, na kosa lake ambalo kwa hilo aliwakosesha Israeli.

Iliyochaguliwa sasa

1 Fal 15: SUV

Kuonyesha

Shirikisha

Nakili

None

Je, ungependa vivutio vyako vihifadhiwe kwenye vifaa vyako vyote? Jisajili au ingia

YouVersion hutumia vidakuzi kubinafsisha matumizi yako. Kwa kutumia tovuti yetu, unakubali matumizi yetu ya vidakuzi kama ilivyoelezwa katika Sera yetu ya Faragha