Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

1 Nya UTANGULIZI

UTANGULIZI
Vitabu viwili viitwavyo vya Mambo ya Nyakati vilikuwa kitabu kimoja katika Biblia ya zamani ya Kiebrania. Viligawanywa katika sehemu mbili na kuwa vitabu viwili baadaye. Mwandishi wake hataji jana lake. Jina la vitabu hivi linatokana na yaliyomo.
Vitabu hivi vinasimulia kwa utaratibu maalumu mambo yaliyokwisha simuliwa katika vitabu vya Yoshua hadi Wafalme pamoja na maandiko mengine (1 Nya 9:1; 27:24; 29:29; 2 Nya 9:29; 12:15; 13:22; 16:11; 20:34; 24:27; 26:22; 27:27: 32:32; 33:18-19). Mwandishi anafasiri matukio kwa fikira na hisia za kiitikadi. Katika hali ya adha anawakumbusha jinsi Mungu alivyowahi kuwatendea, anawatia moyo na kuwapa matumaini ya heri.
Katika kitabu hiki mwandishi anaelezea watu, miongoni mwao ni kama kizazi kipya, misingi ya taifa lao na ya dini yao. Mwandishi anakaza mapokeo ya utawala wa nasaba ya Daudi na maongozi kidini yatokanayo na Makuhani Walawi. Ingawa historia ya taifa la Israeli inasimuliwa, kuna tahadhari kwa wasomaji kuwa wasipotoshwe mifano mibaya ya wakati uliopita. Mamlaka na uwezo wa Daudi, mipango ya ujenzi wa Hekalu la Yerusalemu na huduma ya Walawi ni muhimu katia kitabu hiki.
Yaliyomo:
1. Orodha ya vizazi: Kutoka Adamu hadi Sauli, Sura 1–9
2. Kifo cha Mfalme Sauli, Sura 10
3. Utawala wa Mfalme Daudi, Sura 11–21
4. Matayarisho ya kujenga Hekalu, Sura 22–29

Iliyochaguliwa sasa

1 Nya UTANGULIZI: SUV

Kuonyesha

Shirikisha

Nakili

None

Je, ungependa vivutio vyako vihifadhiwe kwenye vifaa vyako vyote? Jisajili au ingia