Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

1 Nya 5

5
Wazawa wa Reubeni
1 # Mwa 29:32; 49:3; 35:22; 48:15 Na wana wa Reubeni, mzaliwa wa kwanza wa Israeli; (kwa maana ndiye aliyekuwa mzaliwa wa kwanza, lakini, kwa kuwa alikinajisi kitanda cha babaye, haki yake ya mzaliwa wa kwanza walipewa wana wa Yusufu, mwana wa Israeli; tena nasaba isihesabiwe kwa kuifuata hiyo haki ya mzaliwa wa kwanza. 2#Mwa 49:8; Hes 2:3; 7:12; Zab 60:7; 108:8; 78:68-71; Yer 23:5,6; Mik 5:2; Mt 2:6Kwani Yuda ndiye aliyeshinda miongoni mwa nduguze, na kwake ndiko alikotoka mtawala; bali haki ile ya mzaliwa wa kwanza alipewa Yusufu); 3#Mwa 46:9; Kut 6:14; Hes 26:5wana wa Reubeni, mzaliwa wa kwanza wa Israeli; Hanoki, na Palu, na Hesroni, na Karmi. 4Wana wa Yoeli; mwanawe huyo ni Shemaya, na mwanawe huyo ni Gogu, na mwanawe huyo ni Shimei; 5na mwanawe huyo ni Mika, na mwanawe huyo ni Reaya, na mwanawe huyo ni Baali; 6#2 Fal 15:29; 16:7na mwanawe huyo ni Beera, ambaye Tiglath-Pileseri, mfalme wa Ashuru, alimchukua mateka; ndiye aliyekuwa mkuu wa Wareubeni. 7Na nduguze kwa jamaa zao, hapo ilipohesabiwa nasaba ya vizazi vyao; mkuu wao, Yeieli, na Zekaria, 8#Yos 13:15na Bela, mwana wa Azazi, mwana wa Shemaya, mwana wa Yoeli, aliyekaa huko Aroeri, hata kufika Nebo na Baal-meoni; 9#Hes 32:1,33,42; Yos 22:9; Wim 4:1; Mik 7:14na upande wa mashariki akakaa hata kufika maingilio ya jangwa litokalo mto wa Frati; kwa sababu ng’ombe zao walikuwa wameongezeka sana katika nchi ya Gileadi. 10#Mwa 25:12Na katika siku za Sauli wakapigana vita na Wahajiri, ambao waliangushwa kwa mikono yao; nao wakakaa katika hema zao katika nchi yote upande wa mashariki wa Gileadi.
Wazawa wa Gadi
11 # Yos 13:11,24,25 Na wana wa Gadi walikuwa wakikaa kwa kuwaelekea, katika nchi ya Bashani mpaka Saleka; 12Yoeli, alikuwa mkuu wao, na wa pili Shafamu, na Yanai, na Shafati, katika Bashani; 13na ndugu zao wa mbari za baba zao; Mikaeli, na Meshulamu, na Sheba, na Yorai, na Yakani, na Zia, na Eberi, watu saba. 14Hao ndio wana wa Abihaili, mwana wa Huri, mwana wa Yaroa, mwana wa Gileadi, mwana wa Mikaeli, mwana wa Yehishai, mwana wa Yado, mwana wa Buzi; 15Ahi, mwana wa Abdieli, mwana wa Guni, alikuwa mkuu wa mbari za baba zao. 16#1 Nya 27:29; Wim 2:1; Isa 35:2; 65:10Nao wakakaa huko Gileadi, katika Bashani, na katika miji yake, na katika viunga vyote vya Sharoni, hata kufika mipakani mwake. 17#2 Fal 15:5; 14:16,28Hao wote walihesabiwa kwa nasaba, katika siku za Yothamu, mfalme wa Yuda, na siku za Yeroboamu, mfalme wa Israeli.
18Wana wa Reubeni, na Wagadi, na nusu-kabila ya Manase, watu mashujaa, wawezao kuchukua ngao na upanga, na kupiga upinde, wenye ustadi katika kupigana vita, walikuwa watu arobaini na nne elfu mia saba na sitini, walioweza kwenda vitani. 19#Mwa 25:15; 1 Nya 1:31Nao wakapigana vita na Wahajiri; na Yeturi, na Nafishi, na Nodabu. 20#Zab 9:10; 20:7,8; Yer 17:7,8Wakapata msaada juu yao, nao Wahajiri walitiwa mikononi mwao, na wote waliokuwa pamoja nao; kwa kuwa walimlingana Mungu pale vitani; naye akayatakabali maombi yao, kwa sababu walimtumaini yeye. 21Wakateka nyara ng’ombe zao, na ngamia zao hamsini elfu, na kondoo zao mia mbili na hamsini elfu, na punda zao elfu mbili; na watu mia elfu. 22#Kum 20:1,4; Yos 10:42; 2 Nya 20:15; Rum 8:31; 2 Fal 15:29; 17:6Kwani wengi walianguka waliouawa, kwa sababu vita vile vilikuwa vya Mungu. Nao wakakaa badala yao hata wakati wa ule uhamisho.
Nusu Kabila la Manase
23Na wana wa nusu-kabila ya Manase walikaa katika nchi; nao wakaongezeka kutoka Bashani mpaka Baal-hermoni, na Seniri, na mlima Hermoni. 24Na hawa ndio wakuu wa mbari za baba zao; Eferi, na Ishi, na Elieli, na Azrieli, na Yeremia, na Hodavia, na Yadieli; watu hodari wa vita, watu mashuhuri, wakuu wa mbari za baba zao.
25 # Kum 32:15; Isa 1:4; Yer 5:7 Nao wakamwasi Mungu wa baba zao, wakaenda kufanya uasherati na miungu ya watu wa nchi, ambao Mungu alikuwa amewaangamiza mbele yao. 26Naye Mungu wa Israeli akamwamsha roho Pulu, mfalme wa Ashuru na roho ya Tiglath-Pileseri, mfalme wa Ashuru, naye akawachukua mateka hao Wareubeni, na Wagadi, na nusu-kabila ya Wamanase; akawaleta mpaka Hala, na Habori, na Hara, na mpaka mto wa Gozani, hata siku hii ya leo.

Iliyochaguliwa sasa

1 Nya 5: SUV

Kuonyesha

Shirikisha

Nakili

None

Je, ungependa vivutio vyako vihifadhiwe kwenye vifaa vyako vyote? Jisajili au ingia