Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

1 Nya 27

27
Mgawanyo wa Majeshi
1Basi wana wa Israeli kwa hesabu yao, wakuu wa mbari za mababa, na maakida wa maelfu na wa mamia, na wasimamizi wao waliomtumikia mfalme, kwa neno lo lote la zamu za kuingia na za kutoka mwezi kwa mwezi, miezi yote ya mwaka, wa kila zamu, walikuwa watu ishirini na nne elfu. 2#2 Sam 23:8; 1 Nya 11:11Juu ya zamu ya kwanza ya mwezi wa kwanza alikuwa Yashobeamu, mwana wa Zabdieli; na katika zamu yake walikuwa watu ishirini na nne elfu. 3#Mwa 38:29Yeye alikuwa wa wana wa Peresi, mkuu wa maakida wote wa jeshi mwezi wa kwanza. 4#2 Sam 23:9Na juu ya zamu ya mwezi wa pili alikuwa Dodai, Mwahohi, na zamu yake; na Miklothi alikuwa amiri; na katika zamu yake walikuwa watu ishirini na nne elfu. 5#1 Fal 4:5Akida wa tatu wa jeshi mwezi wa tatu alikuwa Benaya, mwana wa Yehoyada, kuhani; alikuwa mkuu, na katika zamu yake walikuwa watu ishirini na nne elfu. 6#2 Sam 23:20-23; 1 Nya 11:22Huyo Benaya ndiye yule aliyekuwa shujaa wa wale thelathini, na juu ya wale thelathini; na katika zamu yake alikuwa Amizabadi mwanawe. 7#2 Sam 2:18,23; 23:24; 1 Nya 11:26Akida wa nne wa mwezi wa nne alikuwa Asaheli, nduguye Yoabu, na Zebadia mwanawe baada yake; na katika zamu yake walikuwa watu ishirini na nne elfu. 8Akida wa tano wa mwezi wa tano alikuwa Shamhuthi, Mwizrahi; na katika zamu yake walikuwa watu ishirini na nne elfu. 9#2 Sam 23:26; 1 Nya 11:28Akida wa sita wa mwezi wa sita alikuwa Ira, mwana wa Ikeshi, Mtekoi; na katika zamu yake walikuwa watu ishirini na nne elfu. 10#1 Nya 11:27Akida wa saba wa mwezi wa saba alikuwa Heksi, Mpeloni, wa wana wa Efraimu; na katika zamu yake walikuwa watu ishirini na nne elfu. 11#2 Sam 21:18; 1 Nya 11:29Akida wa nane wa mwezi wa nane alikuwa Sibekai, Mhushathi, wa Wazera; na katika zamu yake walikuwa watu ishirini na nne elfu. 12#1 Nya 11:28Akida wa kenda wa mwezi wa kenda alikuwa Abiezeri, Mwanathothi, wa Wabenyamini; na katika zamu yake walikuwa watu ishirini na nne elfu. 13#2 Sam 23:28; 1 Nya 11:36Akida wa kumi wa mwezi wa kumi alikuwa Maharai, Mnetofathi, wa Wazera; na katika zamu yake walikuwa watu ishirini na nne elfu. 14#2 Sam 23:30; 1 Nya 11:31Akida wa kumi na moja wa mwezi wa kumi na moja alikuwa Benaya, Mpirathoni, wa wana wa Efraimu; na katika zamu yake walikuwa watu ishirini na nne elfu. 15#1 Nya 11:30; Amu 3:9Akida wa kumi na mbili wa mwezi wa kumi na mbili alikuwa Heledi, Mnetofathi, wa Othnieli; na katika zamu yake walikuwa watu ishirini na nne elfu.
Viongozi wa makabila ya Israeli
16Tena wakuu wa kabila za Israeli walikuwa hawa; wa Wareubeni, Eliezeri mwana wa Zikri; wa Wasimeoni, Shefatia mwana wa Maaka; 17#1 Nya 26:30wa Lawi, Hashabia mwana wa Kemueli; wa Haruni, Sadoki; 18#1 Sam 16:6wa Yuda, Elihu, mmojawapo wa nduguze Daudi; wa Isakari, Omri mwana wa Mikaeli; 19wa Zabuloni, Ishmaya mwana wa Obadia; wa Naftali, Yeromothi mwana wa Azrieli; 20wa wana wa Efraimu, Hoshea mwana wa Azazia, wa nusu kabila ya Manase, Yoeli mwana wa Pedaya; 21wa nusu kabila ya Manase katika Gileadi, Ido mwana wa Zekaria; wa Benyamini, Yaasieli mwana wa Abneri; 22wa Dani, Azareli mwana wa Yerohamu. Hao walikuwa maakida wa kabila za Israeli. 23#Mwa 15:5; Kut 32:13; Kum 1:10; 10:22; Ebr 11:12Lakini Daudi hakufanya hesabu yao wenye miaka ishirini na waliopungua; kwa kuwa BWANA alikuwa amesema, ya kwamba atawaongeza Israeli mfano wa nyota za mbinguni. 24#2 Sam 24:15; 1 Nya 21:7Yoabu, mwana wa Seruya, akaanza kuhesabu, lakini hakumaliza; na ghadhabu ikawapata Israeli kwa hayo; wala haikuhesabiwa hesabu hiyo ndani ya taarifa za mfalme Daudi.
Maofisa Wengine
25Na juu ya hazina za mfalme alikuwa Azmawethi mwana wa Adieli; na juu ya hazina za mashambani, za mijini, na vijijini, na ngomeni, alikuwa Yonathani mwana wa Uzia; 26na juu ya hao wenye kazi ya shamba kuilima ardhi alikuwa Ezri mwana wa Kelubu; 27#Wim 8:11na juu ya mashamba ya mizabibu alikuwa Shimei, Mramathi; na juu ya mazao ya mizabibu kwa ghala za mvinyo alikuwa Zabdi, Mshifmi; 28na juu ya mizeituni na mikuyu iliyokuwamo katika Shefela alikuwa Baal-hanani, Mgederi; na juu ya ghala za mafuta alikuwa Yoashi; 29na juu ya makundi ya ng’ombe waliolishwa katika Sharoni alikuwa Shitrai, Msharoni; na juu ya makundi waliokuwamo mabondeni alikuwa Shafati mwana wa Adlai; 30na juu ya ngamia alikuwa Obili, Mwishmaeli; na juu ya punda alikuwa Yedeya, Mmeronothi; 31na juu ya makundi ya kondoo alikuwa Yazizi, Mhagri. Hao wote walikuwa maakida wa akiba alizokuwa nazo mfalme Daudi.
32 # 2 Sam 21:21 Naye Yonathani, mjombawe Daudi, alikuwa mshauri, na mtu wa akili, na mwandishi; Yehieli mwana wa Hakmoni alikuwa pamoja na wana wa mfalme; 33na Ahithofeli alikuwa mshauri wake mfalme; na Hushai, Mwarki, alikuwa rafiki yake mfalme; 34na, baada ya Ahithofeli, walikuwa Yehoyada mwana wa Benaya, na Abiathari; na jemadari wa jeshi la mfalme alikuwa Yoabu.

Iliyochaguliwa sasa

1 Nya 27: SUV

Kuonyesha

Shirikisha

Nakili

None

Je, ungependa vivutio vyako vihifadhiwe kwenye vifaa vyako vyote? Jisajili au ingia

YouVersion hutumia vidakuzi kubinafsisha matumizi yako. Kwa kutumia tovuti yetu, unakubali matumizi yetu ya vidakuzi kama ilivyoelezwa katika Sera yetu ya Faragha