1 Nya 16:7-13
1 Nya 16:7-13 SUV
Ndipo siku hiyo Daudi alipoagiza kwanza kumshukuru BWANA, kwa mkono wa Asafu na nduguze. Mshukuruni BWANA, liitieni jina lake; Wajulisheni watu matendo yake. Mwimbieni, mwimbieni kwa zaburi; Zitafakarini ajabu zake zote. Jisifuni kwa jina lake takatifu; Na ufurahi moyo wao wamtafutao BWANA. Mtakeni BWANA na nguvu zake; Utafuteni uso wake siku zote. Zikumbukeni ajabu zake alizozifanya; Miujiza yake na hukumu za kinywa chake; Enyi wazao wa Israeli, mtumishi wake, Enyi wana wa Yakobo, wateule wake.