Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

1 Nya 15

15
Sanduku la Agano Laletwa Yerusalemu
1 # 1 Nya 16:1; 17:1-5; Zab 132:2-5; Mdo 7:46 Basi Daudi akajifanyia nyumba katika mji wa Daudi; akapaweka tayari mahali kwa ajili ya sanduku la Mungu, akalipigia hema. 2#Hes 4:2,15; Kum 10:8; 31:9; Yos 3:3Ndipo Daudi akasema, Haimpasi mtu awaye yote kulichukua sanduku la Mungu, isipokuwa Walawi peke yao; kwa kuwa hao ndio aliowachagua BWANA, ili walichukue sanduku la Mungu, na kumtumikia daima. 3#1 Fal 8:1; 1 Nya 13:5Basi Daudi akawakusanya Israeli wote huko Yerusalemu, ili kulipandisha sanduku la BWANA, mpaka mahali pake alipoliwekea tayari. 4Daudi akawakutanisha wana wa Haruni, na Walawi; 5#Kut 6:16-18wa wana wa Kohathi; Urieli mkuu wao, na nduguze mia na ishirini; 6wa wana wa Merari; Asaya mkuu wao, na nduguze mia mbili na ishirini; 7wa wana wa Gershoni; Yoeli mkuu wao, na nduguze mia na thelathini; 8#Kut 6:22wa wana wa Elsafani; Shemaya mkuu wao, na nduguze mia mbili; 9#Kut 6:18; Hes 26:58wa wana wa Hebroni; Elieli mkuu wao, na nduguze themanini; 10wa wana wa Uzieli; Aminadabu mkuu wao, na nduguze mia na kumi na wawili. 11Tena, Daudi akawaita Sadoki na Abiathari makuhani, na hao Walawi, Urieli, Asaya, Yoeli, Shemaya, Elieli, na Aminadabu, 12#Kut 19:10,22; Law 10:3; 1 Sam 7:1; 2 Nya 5:11; 29:5,15; Eze 48:11; Yn 17:17; Rum 12:1,2akawaambia, Ninyi ni vichwa vya mbari za baba za Walawi; jitakaseni, ninyi na ndugu zenu, ili mlipandishe sanduku la BWANA, Mungu wa Israeli, mpaka mahali pale nilipoliwekea tayari. 13#2 Sam 6:3; 1 Nya 13:7,10,11Kwani kwa sababu ninyi hamkulichukua safari ya kwanza, BWANA, Mungu wetu, alitufurikia, kwa maana hatukumtafuta sawasawa na sheria. 14Basi makuhani na Walawi wakajitakasa, ili wapate kulipandisha sanduku la BWANA, Mungu wa Israeli. 15#Kut 25:14; Hes 4:15; 7:9Na wana wa Walawi wakalichukua sanduku la Mungu mabegani mwao kwa miti yake, kama vile Musa alivyoamuru, sawasawa na neno la BWANA. 16#1 Nya 6:31; 13:8; Zab 33:2; 68:25Kisha Daudi akamwambia mkuu wa Walawi, kwamba awaagize ndugu zao waimbaji, pamoja na vyombo vyao vya kupigia ngoma, vinanda, na vinubi, na matoazi, wavipige na kupaza sauti kwa furaha. 17#1 Nya 6:33,39,44Basi Walawi wakamwagiza Hemani mwana wa Yoeli; na wa nduguze, Asafu mwana wa Berekia; na wa wana wa Merari ndugu zao, Ethani mwana wa Kishi; 18na pamoja nao ndugu zao kwa cheo cha pili, Zekaria, na Yaasieli, na Shemiramothi, na Yehieli, na Uni, na Eliabu; na Benaya, na Maaseya, na Matithia, na Elifelehu, na Mikneya, na Obed-edomu, na Yeieli, mabawabu. 19Hivyo hao waimbaji, Hemani, Asafu, na Ethani, wakaagizwa kupiga matoazi yao ya shaba kwa sauti kuu; 20na Zekaria, na Yaasieli na Shemiramothi, na Yehieli, na Uni, na Eliabu, na Maaseya, na Benaya, wenye vinanda vya sauti ya Alamothi; 21na Matithiya, na Elifelehu, na Mikneya, na Obed-edomu, na Yeieli, na Azazia, wenye vinubi vya sauti ya Sheminithi, 22waongoze. Na Kenania, mkuu wa Walawi, alikuwa juu ya uchukuzi; yeye aliusimamia uchukuzi, kwa sababu alikuwa mstadi. 23Na Berekia na Elkana walikuwa mabawabu kwa ajili ya sanduku. 24#Hes 10:8; Zab 81:3Na Shebania, na Yoshafati, na Nethaneli, na Amasai, na Zekaria, na Benaya, na Eliezeri, makuhani, wakapiga baragumu mbele ya sanduku la Mungu; na Obed-edomu na Yehia walikuwa mabawabu kwa ajili ya sanduku. 25#2 Sam 6:12,13; 1 Fal 1:8; Kum 12:7,18; Ezr 6:16Basi Daudi, na wazee wa Israeli, na maakida wa maelfu, wakaenda, ili kulipandisha sanduku la agano la BWANA kutoka nyumbani mwa Obed-edomu kwa furaha kuu; 26#Hes 23:1; Ayu 42:8hata ikawa, Mungu alipowajalia Walawi waliolichukua sanduku la agano la BWANA, wakachinja ng’ombe saba, na kondoo waume saba. 27Naye Daudi alikuwa amevaa joho ya kitani safi, na Walawi wote waliolichukua sanduku, na waimbaji, na Kenania msimamizi wa uchukuzi, na waimbaji; naye Daudi alikuwa amevaa naivera ya kitani. 28#1 Nya 13:8Ndivyo Israeli wote walivyolipandisha sanduku la agano la BWANA kwa shangwe na kwa sauti ya tarumbeta, na kwa baragumu, na kwa matoazi, wakipiga sauti kuu kwa vinanda na vinubi. 29#2 Sam 6:16; Mdo 2:13Hata ikawa, sanduku la agano la BWANA lilipofika mjini kwa Daudi, Mikali binti Sauli akachungulia dirishani, akamwona mfalme Daudi, akicheza na kushangilia; akamdharau moyoni mwake.

Iliyochaguliwa sasa

1 Nya 15: SUV

Kuonyesha

Shirikisha

Nakili

None

Je, ungependa vivutio vyako vihifadhiwe kwenye vifaa vyako vyote? Jisajili au ingia