Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

1 Nya 11

11
Daudi Apakwa Mafuta kuwa Mfalme wa Israeli Wote
1 # 2 Sam 5:1; 1 Nya 12:23 Ndipo Israeli wote wakamkusanyikia Daudi huko Hebroni, wakisema, Tazama, sisi tu mfupa wako na nyama yako. 2#Zab 78:70,71Katika zamani za kale, hata hapo Sauli alipokuwa mfalme, wewe ndiwe uliyewatoa na kuwaingiza Israeli. Naye BWANA, Mungu wako, akakuambia, Ndiwe, utakayewalisha watu wangu Israeli, ndiwe utakayekuwa mkuu juu ya watu wangu Israeli. 3#2 Sam 5:3; Rum 8:31; 1 Sam 16:1Basi wazee wote wa Israeli wakamjia mfalme huko Hebroni; naye Daudi akafanya agano nao huko Hebroni mbele za BWANA; nao wakamtia Daudi mafuta, awe mfalme wa Israeli, sawasawa na neno la BWANA kwa mkono wa Samweli.
Kutekwa kwa Yerusalemu
4 # 2 Sam 5:6; Mwa 10:16; 15:21; Kut 3:17; Amu 1:21; 19:10 Kisha Daudi na Israeli wote wakaenda Yerusalemu, (ndio Yebusi;) nao Wayebusi, wenyeji wa nchi, walikuwamo. 5Na hao wenyeji wa Yebusi wakamwambia Daudi, Hutaingia humu. Walakini Daudi akaitwaa ngome ya Sayuni; huu ndio mji wa Daudi. 6Naye Daudi akasema, Mtu ye yote atakayekuwa wa kwanza wa kuwapiga Wayebusi, yeye atakuwa mkuu na jemadari. Naye wa kwanza aliyepanda ni Yoabu mwana wa Seruya, naye akawa mkuu. 7#2 Sam 5:7Basi Daudi akakaa ngomeni; kwa hiyo huuita mji wa Daudi. 8Akaujenga huo mji pande zote, toka Milo na kuuzunguka; naye Yoabu akautengeneza mji uliosalia. 9Naye Daudi akaendelea, akazidi kuwa mkuu; kwa maana BWANA wa majeshi alikuwa pamoja naye.
Mashujaa wa Daudi na Ushindi wao
10 # 2 Sam 23:8; 1 Sam 16:1,12 Basi hawa ndio wakuu wa mashujaa aliokuwa nao Daudi, waliojitia nguvu pamoja naye katika ufalme wake, pamoja na Israeli wote, ili kumfanya awe mfalme, sawasawa na neno la BWANA alilonena juu ya Israeli. 11Na hii ndiyo hesabu ya hao mashujaa aliokuwa nao Daudi; Yashobeamu, Mhakmoni, mkuu wa maakida; huyo aliuinua mkuki wake juu ya watu mia tatu, akawaua pamoja. 12Na baada yake kulikuwa na Eleazari, mwana wa Dodai, Mwahohi, mmojawapo wa wale mashujaa watatu. 13#1 Sam 17:1Huyo alikuwa pamoja na Daudi huko Pasdamimu; ndiko Wafilisti walikokusanyika vitani,#11:13 Taz. 2 Samweli 23:9-11. palipokuwa na konde limejaa shayiri; na hao watu wakakimbia mbele ya Wafilisti. 14#Mit 21:31Ndipo hao wakasimama katikati ya konde lile, wakalipigania, wakawaua Wafilisti; naye BWANA akafanya wokovu mkuu.
15 # Yos 12:15; 2 Sam 23:13; 1 Nya 14:9; Isa 17:5 Tena, watatu miongoni mwa wale thelathini waliokuwa wakuu wakashuka mwambani, wakamwendea Daudi, hata pango la Adulamu; na jeshi la Wafilisti walikuwa wamefanya kambi bondeni mwa Warefai. 16Na Daudi wakati ule alikuwako ngomeni, na walinzi wa Wafilisti wakati ule walikuwa huko Bethlehemu. 17Naye Daudi akatamani, akasema, Laiti mtu angeninywesha maji ya kisima cha Bethlehemu, kilicho karibu na lango! 18Basi hao watatu wakapenya jeshi la Wafilisti, wakateka maji kutoka kile kisima cha Bethlehemu, kilicho karibu na lango, wakayachukua, wakamletea Daudi; walakini Daudi hakukubali kuyanywa, akayamimina mbele za BWANA; 19akasema, Mungu wangu apishe mbali, nisifanye hivi; je! Ninywe damu ya watu hao waliohatirisha nafsi zao? Maana kwa hatari ya nafsi zao wameyaleta. Kwa hiyo hakukubali kuyanywa. Hayo ndiyo waliyoyafanya wale mashujaa watatu.
20 # 1 Sam 26:6-8; 2 Sam 2:18; 3:20; 18:2; 1 Nya 2:16 Tena Abishai, nduguye Yoabu, alikuwa mkuu wa wale watatu; kwa kuwa aliuinua mkuki wake juu ya watu mia tatu, akawaua; akawa na jina kati ya wale watatu. 21#2 Sam 23:19; 1 Kor 15:41Katika wale watatu yeye alikuwa mwenye heshima kuliko hao wawili, akawa akida wao; ila hakudiriki kuwamo katika wale watatu. 22#2 Sam 1:23; 23:20; 1 Nya 12:8Tena, Benaya, mwana wa Yehoyada, mtu hodari, wa Kabseeli, aliyekuwa amefanya mambo makuu, ndiye aliyewaua simba wakali wawili wa Moabu;#11:22 Au, wana wawili wa Arieli, wa Moabu. pia akashuka, akamwua simba katikati ya shimo wakati wa theluji. 23Huyo akamwua Mmisri, mtu mrefu sana, aliyekuwa wa dhiraa tano urefu wake; na yule Mmisri alikuwa na mkuki kama mti wa mfumaji mkononi; lakini yeye akamshukia na gongo, akamnyakulia Mmisri mkuki mkononi, akamwua kwa mkuki wake mwenyewe. 24Mambo hayo ndiyo aliyoyafanya Benaya, mwana wa Yehoyada, akawa na jina kati ya wale mashujaa watatu. 25Tazama, alikuwa mwenye heshima kuliko wale thelathini, ila hakudiriki kuwamo katika wale watatu; naye Daudi akamweka juu ya walinzi wake.
26 # 2 Sam 2:18-23; 23:24; 1 Nya 27:7 Tena hawa ndio mashujaa wa majeshi ya askari; Asaheli nduguye Yoabu, Elhanani mwana wa Dodo wa Bethlehemu; 27Shama Mharodi, Helesi Mpeloni; 28Ira mwana wa Ikeshi Mtekoi, Abiezeri Mwanathothi; 29Sibekai Mhushathi, Salmoni Mwahohi; 30Maharai Mnetofathi, Heledi mwana wa Baana Mnetofathi; 31Itai mwana wa Ribai wa Gibea wa wana wa Benyamini, Benaya Mpirathoni; 32Hurai wa vijito vya Gaashi, Abieli Mwaibathi; 33Azmawethi Mbaharumi, Eliaba Mshaalboni; 34wana wa Yasheni Mgiloni, Yonathani mwana wa Shama Mharari; 35Ahiamu mwana wa Sharari Mharari, Elifeleti mwana wa Ahasbai; Heferi 36Mmaakathi, Ahia Mpeloni; 37Hezro Mkarmeli, Paarai mwana wa Ezbai Mwarki; 38Yoeli nduguye Nathani, Mibhari mwana wa Hagri; 39Seleki Mwamoni, Naharai Mbeorothi, mchukua silaha wa Yoabu, mwana wa Seruya; 40#Yos 15:48; 1 Nya 2:50,53Ira Mwithri, Garebu Mwithri; 41#2 Sam 11:3Uria Mhiti, Zabadi mwana wa Alai; 42Adina mwana wa Shiza Mreubeni, mkuu wa Wareubeni, na thelathini pamoja naye; 43Hanani mwana wa Maaka, na Yoshafati Mmithni; 44Uzia Mwashterathi, Shama na Yeieli wana wa Hothamu Mwaroeri; 45Yediaeli mwana wa Shimri, na Yoha nduguye, Muzi; 46Elieli Mmahawi, na Yeribai, na Yoshavia, wana wa Elnaamu, na Ithma Mmoabi; 47Elieli, na Obedi, na Yaasieli Mmesobai.

Iliyochaguliwa sasa

1 Nya 11: SUV

Kuonyesha

Shirikisha

Nakili

None

Je, ungependa vivutio vyako vihifadhiwe kwenye vifaa vyako vyote? Jisajili au ingia

YouVersion hutumia vidakuzi kubinafsisha matumizi yako. Kwa kutumia tovuti yetu, unakubali matumizi yetu ya vidakuzi kama ilivyoelezwa katika Sera yetu ya Faragha