Sefania Utangulizi
Utangulizi
Jina “Sefania” maana yake ni “Aliyefichwa na Yehova”. Sefania alikuwa wa ukoo wa Hezekia, mfalme wa Yuda. Nabii Sefania alihudumu wakati wa utawala wa Mfalme Yosia (mwaka 636–609 K.K). Sefania alionya kwamba siku ya Bwana ingeleta hukumu kwa Yuda pamoja na Yerusalemu, hivyo akawashauri Wayahudi kumrudia Mwenyezi Mungu. Uvamizi wa kuteka Yuda ulikuwa unakuja kutoka kaskazini, nao ungeyakumba pia mataifa yaliyowazunguka. Ingawa hukumu ya Yuda imeainishwa, ahadi ya kufanywa upya ni yakini. Mataifa yatahukumiwa na kutiishwa na mfalme wa Israeli, atakayetawala kutoka Sayuni.
Mwandishi
Sefania.
Kusudi
Kuwaonya watu wa Yuda kuacha ibada ya sanamu na maovu yote na kumrudia Mwenyezi Mungu.
Mahali
Yerusalemu.
Tarehe
Mnamo 640–609 K.K.
Wahusika Wakuu
Sefania, na watu wa Yuda.
Wazo Kuu
Sefania aliwapa watu matumaini kwamba Mwenyezi Mungu angewarudisha watu wake nyumbani.
Mambo Muhimu
Hukumu na urejesho kwa watu wa Yuda.
Yaliyomo
Kutangazwa kwa hukumu ya Mwenyezi Mungu (1:1–2:3)
Hukumu dhidi ya mataifa (2:4-15)
Maisha ya baadaye ya Yerusalemu (3:1-20).
Iliyochaguliwa sasa
Sefania Utangulizi: NENO
Kuonyesha
Shirikisha
Nakili

Je, ungependa vivutio vyako vihifadhiwe kwenye vifaa vyako vyote? Jisajili au ingia
Neno: Maandiko Matakatifu™ NMM™
Hakimiliki © 2018, 2024 na Biblica, Inc.
Imetumiwa kwa ruhusa.
Haki zote zimehifadhiwa duniani kote.
Kiswahili Contemporary Scriptures™
Copyright © 2018, 2024 by Biblica, Inc.
Used with permission. All rights reserved worldwide.