Zekaria Utangulizi
Utangulizi
Maana ya jina Zekaria ni “Mwenyezi Mungu amekumbuka”. Zekaria alikuwa kijana wakati alipoanza huduma yake. Zekaria aliwaonya watu waliokuwa wameanza kujenga upya Hekalu kwamba iliwapasa kusikiliza ujumbe wa Mwenyezi Mungu kupitia kwa manabii. Aliwahimiza kudumisha uhusiano na Mwenyezi Mungu ili wasiiharakishe hukumu ya Mwenyezi Mungu. Maono ya nabii Zekaria yalikuwa ya kuwatia moyo wajenzi katika wakati mgumu, na kuwahakikishia kwamba Mwenyezi Mungu alikuwa na mpango wa muda mrefu kwa ajili ya Israeli.
Sehemu ya mwisho ya huduma yake, Zekaria alikazia mpango wa maendeleo wa muda mrefu, akionesha kuanzishwa kwa ufalme wa mwisho. Mfalme anatambulishwa kama anayekuja kwa unyenyekevu akileta wokovu, lakini akikataliwa na watu wake mwenyewe, yaani Waisraeli. Mataifa yatakapokusanyika kwa ajili ya vita dhidi ya Yerusalemu, Waisraeli watamtambua Masihi na wataibuka na ushindi, nayo mataifa yote yatakuja Yerusalemu kumwabudu Mfalme.
Mwandishi
Zekaria.
Kusudi
Kuwatia moyo Waisraeli na kuwajulisha mpango wa Mungu wa baadaye wa ukombozi kupitia kwa Masihi.
Mahali
Yerusalemu.
Tarehe
Sura 1–8: mnamo 520–518 K.K.; sura 9–14: mnamo 480–470 K.K.
Wahusika Wakuu
Zekaria, Zerubabeli, Yoshua na Wayahudi waliorudi kutoka uhamishoni.
Wazo Kuu
Ahadi za Masihi na kumalizia ujenzi wa Hekalu.
Mambo Muhimu
Zekaria alieleza juu ya hukumu ya Mwenyezi Mungu dhidi ya adui za Israeli, baraka kwa ajili ya Yerusalemu, na umuhimu wa watu wa Mwenyezi Mungu kudumu katika utakatifu. Mwenyezi Mungu atawahukumu adui wa Israeli, na Mfalme (yaani Masihi) atakuja.
Yaliyomo
Utangulizi (1:1-6)
Maono nane ya kinabii (1:7–6:8)
Kutawazwa kwa Yoshua kinabii (6:9-15)
Jumbe mbalimbali za hukumu na matumaini (7:1–11:3)
Kuja kwa Masihi na kukataliwa kwake (11:4–13:9)
Mwenyezi Mungu yuaja kutawala (14:1-21).
Iliyochaguliwa sasa
Zekaria Utangulizi: NENO
Kuonyesha
Shirikisha
Nakili

Je, ungependa vivutio vyako vihifadhiwe kwenye vifaa vyako vyote? Jisajili au ingia
Neno: Maandiko Matakatifu™ NMM™
Hakimiliki © 2018, 2024 na Biblica, Inc.
Imetumiwa kwa ruhusa.
Haki zote zimehifadhiwa duniani kote.
Kiswahili Contemporary Scriptures™
Copyright © 2018, 2024 by Biblica, Inc.
Used with permission. All rights reserved worldwide.