Zekaria 2:1-5
Zekaria 2:1-5 NENO
Kisha nikatazama juu: pale mbele yangu palikuwa na mtu mwenye kamba ya kupimia mkononi mwake! Nikamuuliza, “Unaenda wapi?” Akanijibu, “Kupima Yerusalemu, kupata urefu na upana wake.” Kisha malaika aliyekuwa akizungumza nami akaondoka, malaika mwingine akaja kukutana naye na kumwambia: “Kimbia, umwambie yule kijana, ‘Yerusalemu utakuwa mji usio na kuta kwa sababu ya wingi wa watu na mifugo iliyomo. Mimi mwenyewe nitakuwa ukuta wa moto kuuzunguka,’ asema Mwenyezi Mungu, ‘nami nitakuwa utukufu wake ndani yake.’