Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Ruthu 1:19-22

Ruthu 1:19-22 NEN

Kwa hiyo hao wanawake wawili wakaondoka, wakafika Bethlehemu. Walipofika Bethlehemu, mji mzima ulitaharuki, wanawake wakashangaa, wakasema, “Huyu aweza kuwa ni Naomi?” Akawaambia, “Msiniite tena Naomi, niiteni Mara, kwa sababu Mwenyezi amenitendea mambo machungu sana. Mimi niliondoka hali nimejaa, lakini BWANA amenirudisha mtupu. Kwa nini kuniita Naomi? BWANA amenitendea mambo machungu; Mwenyezi ameniletea msiba.” Kwa hiyo Naomi alirudi pamoja na Ruthu Mmoabu mkwe wake, nao wakafika Bethlehemu mwanzoni mwa kuvuna shayiri.

Mipango ya Kusoma Bila Malipo na Ibada zinazohusiana na Ruthu 1:19-22