Warumi 14:16-18
Warumi 14:16-18 NEN
Usiruhusu kile ambacho unakiona kuwa chema kisemwe kuwa ni kiovu. Kwa maana Ufalme wa Mungu si kula na kunywa, bali ni haki, amani na furaha katika Roho Mtakatifu. Kwa sababu mtu yeyote anayemtumikia Kristo kwa jinsi hii, anampendeza Mungu na kukubaliwa na wanadamu.