Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Warumi 12:14-21

Warumi 12:14-21 NEN

Wabarikini wale wanaowatesa, barikini wala msilaani. Furahini pamoja na wenye kufurahi, lieni pamoja na wale waliao. Kaeni kwa amani ninyi kwa ninyi. Msijivune, bali mwe tayari kushirikiana na wanyonge. Wala msiwe watu wenye kujivuna kwamba mnajua kila kitu. Msimlipe mtu yeyote ovu kwa ovu. Jitahidini ili mtende yaliyo mema machoni pa watu wote. Kama ikiwezekana, kwa upande wenu kaeni kwa amani na watu wote. Wapendwa, msilipize kisasi, bali ipisheni ghadhabu ya Mungu, maana imeandikwa: “Ni juu yangu kulipiza kisasi, nitalipiza,” asema Bwana. Badala yake: “Kama adui yako ana njaa, mlishe; kama ana kiu, mpe kinywaji. Kwa kufanya hivyo, unaweka makaa ya moto yanayowaka kichwani pake.” Usishindwe na ubaya, bali uushinde ubaya kwa wema.

Video for Warumi 12:14-21

Mipango ya Kusoma Bila Malipo na Ibada zinazohusiana na Warumi 12:14-21