Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Ufunuo 16

16
Mabakuli saba ya ghadhabu ya Mwenyezi Mungu
1Kisha nikasikia sauti kubwa kutoka mle Hekaluni ikiwaambia wale malaika saba, “Nendeni, mkayamwage duniani hayo mabakuli saba ya ghadhabu ya Mungu.”
2Malaika wa kwanza akaenda akalimwaga hilo bakuli lake juu ya nchi. Majipu mabaya yenye maumivu makali yakawapata wale watu wote waliokuwa na chapa ya yule mnyama na walioabudu sanamu yake.
3Malaika wa pili akalimwaga bakuli lake baharini, nayo ikabadilika kuwa damu kama ya mtu aliyekufa na kila kiumbe hai kilichokuwa ndani ya bahari kikafa.
4Malaika wa tatu akalimwaga bakuli lake katika mito na chemchemi za maji, nazo zikawa damu. 5Ndipo nikamsikia malaika msimamizi wa maji akisema:
“Wewe una haki katika hukumu hizi ulizotoa,
wewe uliyeko, uliyekuwako, Uliye Mtakatifu,
kwa sababu umehukumu hivyo;
6kwa kuwa walimwaga damu ya watakatifu wako
na manabii wako,
nawe umewapa damu wanywe
kama walivyostahili.”
7Nikasikia madhabahu ikiitikia,
“Naam, Bwana Mungu Mwenyezi,
hukumu zako ni kweli na haki.”
8Malaika wa nne akamimina bakuli lake kwenye jua, nalo likapewa nguvu za kuwaunguza watu kwa moto. 9Watu wakaunguzwa na hilo joto kali, wakalaani Jina la Mungu, aliyekuwa na uwezo juu ya mapigo haya, tena wakakataa kutubu na kumtukuza Mungu.
10Malaika wa tano akamimina bakuli lake kwenye kiti cha utawala cha yule mnyama, nao ufalme wake ukagubikwa na giza. Watu wakatafuna ndimi zao kwa ajili ya maumivu, 11wakamlaani Mungu wa mbinguni kwa sababu ya maumivu na majeraha yao, wala hawakutubu kwa ajili ya matendo yao maovu.
12Malaika wa sita akamimina bakuli lake kwenye mto mkubwa Frati, maji yake yakakauka ili kutayarisha njia kwa ajili ya wafalme kutoka Mashariki. 13Kisha nikaona roho wachafu watatu waliofanana na vyura wakitoka katika kinywa cha lile joka na katika kinywa cha yule mnyama na katika kinywa cha yule nabii wa uongo. 14Hizo ndizo roho za pepo wachafu zitendazo miujiza. Nazo huwaendea wafalme wa ulimwengu wote na kuwakusanya tayari kwa ajili ya vita katika siku ile kuu ya Mungu Mwenyezi.
15“Tazama, naja kama mwizi! Amebarikiwa yeye akeshaye na kuziweka tayari nguo zake ili asiende uchi na kuonekana aibu yake.”
16Ndipo wakawakusanya wafalme pamoja mahali paitwapo Har-Magedoni kwa Kiebrania.
17Malaika wa saba akamimina bakuli lake angani na sauti kubwa ikatoka mle Hekaluni katika kile kiti cha enzi, ikisema, “Imekwisha kuwa!” 18Kukawa na miali ya radi, ngurumo, radi na tetemeko kubwa la ardhi. Hapajawahi kuwa na tetemeko la ardhi kama hilo tangu mwanadamu awepo duniani, kwani lilikuwa tetemeko kubwa ajabu. 19Ule mji mkubwa ukagawanyika katika sehemu tatu, nayo miji ya mataifa ikaanguka. Mungu akakumbuka Babeli Mkuu na kumpa kikombe kilichojaa mvinyo wa ghadhabu ya hasira yake. 20Kila kisiwa kikatoweka wala milima haikuonekana. 21Mvua kubwa ya mawe yenye uzito wa talanta moja#16:21 Talanta moja ni kama kilo 34. ikashuka kutoka mbinguni, ikawaangukia wanadamu. Nao wanadamu wakamlaani Mungu kwa ajili ya hayo mapigo ya mvua ya mawe, kwa sababu pigo hilo lilikuwa la kutisha.

Iliyochaguliwa sasa

Ufunuo 16: NENO

Kuonyesha

Shirikisha

Nakili

None

Je, ungependa vivutio vyako vihifadhiwe kwenye vifaa vyako vyote? Jisajili au ingia