Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Zaburi 99:5-9

Zaburi 99:5-9 NEN

Mtukuzeni BWANA Mungu wetu, na mkaabudu katika mahali pa kuwekea miguu yake; yeye ni mtakatifu. Mose na Aroni walikuwa miongoni mwa makuhani wake, Samweli alikuwa miongoni mwa walioliitia jina lake; walimwita BWANA, naye aliwajibu. Alizungumza nao kutoka nguzo ya wingu; walizishika sheria zake na amri alizowapa. Ee BWANA, wetu, ndiwe uliyewajibu, kwa Israeli ulikuwa Mungu mwenye kusamehe, ingawa uliadhibu matendo yao mabaya. Mtukuzeni BWANA Mungu wetu, mwabuduni kwenye mlima wake mtakatifu, kwa maana BWANA Mungu wetu ni mtakatifu.