Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Zaburi 98

98
Zaburi 98
Mungu Mtawala Wa Dunia
Zaburi.
1 Mwimbieni Bwana wimbo mpya,
kwa maana ametenda mambo ya ajabu;
kitanga chake cha kuume na mkono wake mtakatifu
umemfanyia wokovu.
2 Bwana ameufanya wokovu wake ujulikane
na amedhihirisha haki yake kwa mataifa.
3 Ameukumbuka upendo wake
na uaminifu wake kwa nyumba ya Israeli;
miisho yote ya dunia imeuona
wokovu wa Mungu wetu.
4 Mpigieni Bwana kelele za shangwe, dunia yote,
ipaze sauti kwa nyimbo za shangwe na vinanda;
5 mwimbieni Bwana kwa kinubi,
kwa kinubi na sauti za kuimba,
6 kwa tarumbeta na mvumo wa baragumu za pembe za kondoo dume:
shangilieni kwa furaha mbele za Bwana, aliye Mfalme.
7 Bahari na ivume na kila kiliomo ndani yake,
dunia na wote wakaao ndani yake.
8 Mito na ipige makofi,
milima na iimbe pamoja kwa furaha,
9 vyote na viimbe mbele za Bwana,
kwa maana yuaja kuhukumu dunia.
Atahukumu dunia kwa haki
na mataifa kwa haki.

Iliyochaguliwa sasa

Zaburi 98: NEN

Kuonyesha

Shirikisha

Nakili

None

Je, ungependa vivutio vyako vihifadhiwe kwenye vifaa vyako vyote? Jisajili au ingia

YouVersion hutumia vidakuzi kubinafsisha matumizi yako. Kwa kutumia tovuti yetu, unakubali matumizi yetu ya vidakuzi kama ilivyoelezwa katika Sera yetu ya Faragha