Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Zaburi 96:7-13

Zaburi 96:7-13 NEN

Mpeni BWANA, enyi jamaa za mataifa, mpeni BWANA utukufu na nguvu. Mpeni BWANA utukufu unaostahili jina lake; leteni sadaka na mje katika nyua zake. Mwabuduni BWANA katika uzuri wa utakatifu wake; dunia yote na itetemeke mbele zake. Katikati ya mataifa semeni, “BWANA anatawala.” Ulimwengu ameuweka imara, hauwezi kusogezwa; atawahukumu watu kwa uadilifu. Mbingu na zishangilie, nchi na ifurahi; bahari na ivume, na vyote vilivyomo ndani yake; mashamba na yashangilie, pamoja na vyote vilivyomo ndani yake. Kisha miti yote ya msituni itaimba kwa furaha; itaimba mbele za BWANA kwa maana anakuja, anakuja kuihukumu dunia. Ataihukumu dunia kwa haki, na mataifa katika kweli yake.