Zaburi 86:11-17
Zaburi 86:11-17 NENO
Ee Mwenyezi Mungu, nifundishe njia yako, nami nitaenda katika kweli yako; nipe moyo usiositasita, ili niweze kulicha jina lako. Ee Mwenyezi Mungu, Mungu wangu, nitakusifu kwa moyo wote; nitaliadhimisha jina lako milele. Kwa maana upendo wako ni mkuu kwangu; umeniokoa kutoka vilindi vya kaburi. Ee Mungu, wenye majivuno wananishambulia; kundi la watu wakatili linatafuta uhai wangu: watu wasiokuheshimu wewe. Lakini wewe, Ee Bwana, ni Mungu wa huruma na neema, si mwepesi wa hasira, bali ni mwingi wa upendo na uaminifu. Nigeukie na unihurumie; mpe mtumishi wako nguvu zako, mwokoe mwana wa mjakazi wako. Nipe ishara ya wema wako, ili adui zangu waione nao waaibishwe, kwa kuwa wewe, Ee Mwenyezi Mungu, umenisaidia na kunifariji.