Zaburi 85
85
Zaburi 85
Maombi kwa ajili ya ustawi wa taifa
Kwa mwimbishaji. Zaburi ya wana wa Kora.
1Ee Mwenyezi Mungu, ulionesha wema kwa nchi yako.
Ulimrejeshea Yakobo baraka zake.#85:1 au Uliwarudisha mateka wa Yakobo.
2Ulisamehe uovu wa watu wako,
na kufunika dhambi zao zote.
3Uliweka kando ghadhabu yako yote
na umegeuka na kuiacha hasira yako kali.
4Ee Mungu Mwokozi wetu, uturejeshe tena,
nawe uiondoe chuki yako juu yetu.
5Je, utatukasirikia milele?
Utaendeleza hasira yako kwa vizazi vyote?
6Je, hutatuhuisha tena,
ili watu wako wakufurahie?
7Utuoneshe upendo wako usiokoma, Ee Mwenyezi Mungu,
utupe wokovu wako.
8Nitasikiliza lile atakalosema Mungu aliye Mwenyezi Mungu;
anaahidi amani kwa watu wake, watakatifu wake:
lakini nao wasirudie upumbavu.
9Hakika wokovu wake uko karibu na wale wamchao,
ili utukufu wake udumu katika nchi yetu.
10Upendo na uaminifu hukutana pamoja,
haki na amani hubusiana.
11Uaminifu huchipua kutoka nchi,
haki hutazama chini kutoka mbinguni.
12Naam, hakika Mwenyezi Mungu atatoa kilicho chema,
nayo nchi yetu itazaa mavuno yake.
13Haki itatangulia mbele yake
na kutengeneza njia kwa ajili ya hatua zake.
Iliyochaguliwa sasa
Zaburi 85: NENO
Kuonyesha
Shirikisha
Nakili

Je, ungependa vivutio vyako vihifadhiwe kwenye vifaa vyako vyote? Jisajili au ingia
Neno: Maandiko Matakatifu™ NMM™
Hakimiliki © 2018, 2024 na Biblica, Inc.
Imetumiwa kwa ruhusa.
Haki zote zimehifadhiwa duniani kote.
Kiswahili Contemporary Scriptures™
Copyright © 2018, 2024 by Biblica, Inc.
Used with permission. All rights reserved worldwide.