Zaburi 69:9-15
Zaburi 69:9-15 NEN
Kwa kuwa wivu wa nyumba yako unanila, matukano ya wale wanaokutukana yameniangukia. Ninapolia na kufunga, lazima nivumilie matusi. Ninapovaa nguo ya gunia, watu hunidharau. Wale wanaoketi mlangoni wananisimanga, nimekuwa wimbo wa walevi. Lakini Ee BWANA, ninakuomba, kwa wakati ukupendezao; katika upendo wako mkuu, Ee Mungu, unijibu kwa wokovu wako wa hakika. Uniokoe katika matope, usiniache nizame; niokoe na hao wanichukiao, kutoka kwenye vilindi vya maji. Usiache mafuriko yanigharikishe au vilindi vinimeze, au shimo lifumbe kinywa chake juu yangu.