Zaburi 6
6
Zaburi 6
Sala ya kuomba msaada wakati wa taabu
Kwa mwimbishaji. Kwa ala za nyuzi za muziki. Mtindo wa sheminithi.#6:0 Sheminithi ni mtajo mojawapo katika lugha ya uimbaji. Zaburi ya Daudi.
1Ee Mwenyezi Mungu, usinikemee katika hasira yako,
wala usiniadhibu katika ghadhabu yako.
2Unirehemu Mwenyezi Mungu,
kwa maana nimedhoofika;
Ee Mwenyezi Mungu, uniponye,
kwa maana mifupa yangu
ina maumivu makali.
3Nafsi yangu ina uchungu mwingi.
Hadi lini, Ee Mwenyezi Mungu, hadi lini?
4Geuka, Ee Mwenyezi Mungu, unikomboe,
uniokoe kwa sababu ya fadhili zako.
5Hakuna mtu anayekukumbuka
akiwa amekufa.
Ni nani awezaye kukusifu
akiwa Kuzimu#6:5 Kuzimu kwa Kiebrania ni Sheol, yaani Shimo lisilo na mwisho.?
6Nimechakaa kwa kulia kwa huzuni;
usiku kucha natiririsha
kitanda changu kwa machozi;
nimelowesha kiti changu
kwa machozi yangu.
7Macho yangu yamedhoofika kwa kuhuzunika,
yamedhoofika kwa sababu ya adui zangu wote.
8Kaeni mbali nami, ninyi nyote mtendao mabaya,
kwa maana Mwenyezi Mungu amesikia kulia kwangu.
9Mwenyezi Mungu amesikia kilio changu kwa huruma,
Mwenyezi Mungu amekubali sala yangu.
10Adui zangu wote wataaibika na kufadhaika,
watarudi nyuma na waaibishwe kwa ghafula.
Iliyochaguliwa sasa
Zaburi 6: NENO
Kuonyesha
Shirikisha
Nakili

Je, ungependa vivutio vyako vihifadhiwe kwenye vifaa vyako vyote? Jisajili au ingia
Neno: Maandiko Matakatifu™ NMM™
Hakimiliki © 2018, 2024 na Biblica, Inc.
Imetumiwa kwa ruhusa.
Haki zote zimehifadhiwa duniani kote.
Kiswahili Contemporary Scriptures™
Copyright © 2018, 2024 by Biblica, Inc.
Used with permission. All rights reserved worldwide.