Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Zaburi 44:1-8

Zaburi 44:1-8 NEN

Ee Mungu, tumesikia kwa masikio yetu, baba zetu wametueleza yale uliyotenda katika siku zao, siku za kale. Kwa mkono wako uliwafukuza mataifa na ukawapanda baba zetu, uliangamiza mataifa na kuwastawisha baba zetu. Sio kwa upanga wao waliipata nchi, wala si mkono wao uliwapatia ushindi; ilikuwa ni kitanga cha mkono wako wa kuume, na nuru ya uso wako, kwa kuwa uliwapenda. Wewe ni mfalme wangu na Mungu wangu, unayeamuru ushindi kwa Yakobo. Kwa uwezo wako tunawasukuma nyuma watesi wetu; kwa jina lako tunawakanyaga adui zetu. Siutumaini upinde wangu, upanga wangu hauniletei ushindi; bali wewe unatupa ushindi juu ya adui zetu, unawaaibisha watesi wetu. Katika Mungu wetu tunajivuna mchana kutwa, nasi tutalisifu jina lako milele.