Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Zaburi 40:1-8

Zaburi 40:1-8 NENO

Nilimngoja Mwenyezi Mungu kwa saburi, naye akanijia na kusikia kilio changu. Akanipandisha kutoka shimo la uharibifu, kutoka matope na utelezi; akaiweka miguu yangu juu ya mwamba na kunipa mahali imara pa kusimama. Akaweka wimbo mpya kinywani mwangu, wimbo wa sifa kwa Mungu wetu. Wengi wataona na kuogopa na kuweka tumaini lao kwa Mwenyezi Mungu. Heri mtu yule amfanyaye Mwenyezi Mungu kuwa tumaini lake, asiyewategemea wenye kiburi, wale wenye kugeukia miungu ya uongo. Ee Mwenyezi Mungu, Mungu wangu, umefanya mambo mengi ya ajabu. Mambo uliyopanga kwa ajili yetu hakuna awezaye kukuhesabia; kama ningesema na kuyaelezea, yangekuwa mengi mno kuyatangaza. Dhabihu na sadaka hukuvitaka, lakini umefungua masikio yangu; sadaka za kuteketezwa na sadaka za dhambi hukuzihitaji. Ndipo niliposema, “Mimi hapa, nimekuja: imeandikwa kunihusu katika kitabu. Ee Mungu wangu, natamani kuyafanya mapenzi yako; sheria yako iko ndani ya moyo wangu.”